
Huyu
ndie Naomi James ambaye ametawazwa usiku huu kuwa Miss Redd's mkoa
wa Iringa na kuzawadiwa kitita cha shilingi 500,000

Mshindi
wa taji la Miss REdd's 2012 mkoa wa Iringa Naomi James kati kati
akiwa na mshindi wa pili Sarah Utiku na Catherine Mfupi ambaye ni
mshindi wa tatu mara baada ya kutangazwa usiku huu ndani ya ukumbi
wa Highlands mjini Iringa

Msaidizi
wa chifu jaji msomi Saimon Belenge akiokoa jahazi lisizame baada
ya wadau wapenzi na mashabiki wa onyesho hilo kuanza kumzomea chifu
jaji Bw Tasha Jimi ambaye ni mratibu wa Miss Redd's mikoa ya kusini
baada ya kuchemka kutaja namba ya mshindi wa pili katika onyesho
hilo

Hawa
ndio waliopenya nafasi ya tano bora kati ya washiriki 12 waliopanda
jukwani wa kwanza kushoto ni Amisa Zuber, SArah Utiku, Naomi James
,Winfreda Felix na Catherine Mfupi

Wadau
wa urembo leo wakiwa wamevalia nguo za heshima kiasi

Warembo
wakiwa katika picha ya pamoja na washindi na washiriki wa onyesho
hilo

Mgeni
rasimi Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki ( wa pili
kushoto) akiwa na afisa michezo na utamaduni Manispaa ya Iringa
Bw.Kadinde na mratibu wa onyesho hilo Bw Dosi

Hawa
ndio majaji wa onyesho hilo katikati ni Tasha Jimbo aliyetaka
kuvuruga onyesho dakika za mwisho

Msomi
Saimon Belege (kulia) akicheka baada ya chifu jaji kushoto
TashaJimy kuvuruga kazi yao


Madau
Saimon Belege akiwa na mshindi wa taji la Miss Iringa mwaka jana na
mshindi wa leo katika shindano ya Redd's Miss Iringa Naomi James


Huyu
ndiye Tasha Jimy aliyezomewa kwa kushindwa kujua tofauti kati ya
namba 4 na mbili hivyo kujikuta akizomewa ukumbini.
Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni Dokta FENELLA
MUKANGARA(pichani) amepata ajali ya gari katika Wilaya ya Nzega Mkoani
Tabora akiwa njiani kwenda Mkoani Mwanza kikazi.
Habari
kutoka Wilayani Nzega zinasema kwamba ajali hiyo imetokea leo asubuhi
wakati Waziri huyo akiwa njiani akitokea Dodoma kwenda Mkoani Mwanza
kuzindua Mashindano ya Vishale.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kwamba
gari aliyokuwa amepanda Waziri MUKANGARA akiwa na Msaidizi wake
imepinduka mara Tatu na inadaiwa kuwa Waziri huyo ameumia Mguu wa
kushoto na amekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega kwa ajili ya
matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment