WAKATI madaktari wa hospitali za serikali nchini wameweka ngumu kutibu
wagonjwa wakidai kuboreshewa mishahara, baadhi ya waganga wa kienyeji
wameonekana kufurahia kwa sababu sasa wanapata wagonjwa wengi wanaotaka
tiba kwao.
Waganga wa jadi wametakiwa kutoa huduma bora na kwa umakini
zaidi ili kulinda afya za wagonjwa wao pamoja na zao pia.
Hayo yamesemwa na katibu wa kamati tendaji ya mkoa wa Iringa dkt
Maiko Evaristo Kalinga katika semina ya waganga wa jadi na wakunga iliyofanyika
ukumbi wa Siasa ni Kilimo manispaa ya Iringa. Waganga hao wametakiwa kutumia
njia za kisasa kama uuvaaji wa glovu ili kuzuia maambukizi ya magonjwa, pia
kuboresha maeneo yao
ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwa wasafi.
Pia amewataka waganga hao kutoa tiba na kuacha kupiga lamli
kwani ni chanzo cha ugomvi na mauji katika jamii.
Akiendelea kutoa mafunzo hayo amewataka watendaji wa kata na
vijiji ambao wamekuwa wakiwapokea waganga wa jadi bila utaratibu maalum kuacha
tabia hiyo. Kwani wamekuwa wakiwapokea waganga
ambao ni matapeli.
Pia ametoa onyo kwa wakunga wa jadi kuwa hawaruhusiwi kutoa
dawa za asili kwa kina mama wajawazito kwani wamekuwa wakichangia kwa kiasi
kikubwa vifo vya watoto wachanga na kina mama, badala yake wametakiwa kutoa
ushari kwa wajawazito kuhudhuria hospitali.
Naye mratibu wa waganga wa jadi mkoa wa iringa Ibrahim
Kamisa amewasomea masharti ambayo serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa
jamii wameweka sheria kwa waganga hao wa
jadi.
Semina hiyo iliambatana na ugawaji wa lesini kwa waganga 19
wa jadi ambao wamekwisha sajiliwa. Akigawa leseni hizo mkuu wa wilaya dokta Leticia Warioba amesema kuwa waganga
hao wanatakiwa kushirikiana katika shughuli zao, wawe wasafi na kutoa ushauri
kwa wagonjwa waende hospitali mapema pale wanaposhindwa kuwatibia.
Pia amewapongeza waganga waliopewa leseni na kutoa wito kwa
waganga ambao hawajasajiliwa kujisajili
mapema ili nao waweze kupewa leseni
No comments:
Post a Comment