ASKOFU BOAZ SOLLO AENDELEA KUITIKISA IRINGA KATIKA HUDUMA YA OVERCOMERS POWER CENTRE NA HUDUMA YA OVERCOMERS HOUR KINACHORUSHWA NA REDIO OVERCOMERS FM 98.6 SAA TATU KAMILI HADI SAA NNE KAMILI USIKU,WAGONJWA NAWENYE SHIDA MBALIMBALI WAENDELEA KUFUNGULIWA
Zifuatazo ni Picha za wakati wa huduma yake
Askofu.Dk Boaz Sollo akisoma neno katika ibada |
Askofu.Dk Boaz Sollo akiombea wagonjwa leo Alhamisi Iringa |
Mwimbaji Shiza Shadrack Sanga akiimba katika ibada Overcomers Power Centre leo Alhamis |
Waumini waliohudhuria katika ibada Overcomers Power Centre Iringa mjini |
KIJIJI CHA UDEKWA CHAINGI KATIKA MGOGORO WA KISIASA ,MAENDELEO CHANZO
Mwenyekiti wa kijiji cha Udekwa wilayani Kilolo mkoani Iringa bwana Obadia Lubago amelalamikia kitendo cha Mkuu wa wilaya hiyo bwana Gulimitu kuingilia shughuli zaq maendelea zinazofanywa na wananchi wa kijiji hicho zinazosimamiwa na mwenyekiti huyo kitendo ambacho wamedai ni kutokana na mkuu huyo wa wilaya kutokea katika Chama cha Mapinduzi ambapo amesema yeye hatambui shughuli zinazofanywa na mwenyekiti huyo wa mtaa na kusema kuwa hata kama anasimamia maendeleo ya wananchi lakini anatakiwa kuteleza sera na ilani ya Chama Cha Mapindu (CCM) kwa kuwa woa ndio vijogoo wa nchi vyama vingine ni Uchwara tu kauli ambayo imemsononesha kwa kiasi kikubwa mwenyekiti huyo.Malalamiko hayo yamekuja baada ya mkuu huyo wa wilaya ya kilolo bwana Gerad Guninira kufanya ziara katika kijiji hicho cha Udekwe ziara ambayo iliwapa matumaini Viongozi na wananchi wa kijiji hicho kuwa ujio wa mkuu huyo utafufua matumaini ya mazungumzo yao juu ya changamoto zinazowakabili wananchi wa kijiji hicho hali ambayo ilikuwa ndivyo sivyo baada ya mkuu huyo wa wilaya kusomewa taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji na ndipo ilipofika zamu ya mkuu wa wilaya kusoma taarifa yake pamoja na kujibu hoja za taarifa ya kijiji liyotumia takribani saa zima akizungumza na ndipo alipo maliza mkutano na wanakijiji aliwaita viongo wa kijiji wakiwemo Madiwani,Wenyeviti katika kikao na ndipo alipojaribu kutumia fursa hiyo kuwa sema na kuwa sakama viongozi hao
Pia hali hiyo ilitokana na wananchi wa Udekwa kushindwa kuchangia mchango wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2012 uliopangwa kupita katika kijiji hicho ambapo kila kijiji katika wilaya hiyo ya Kilolo kutakiwa kuchangia kiasi cha shilingi 70,000/= kitendo ambacho wananchi hao walishindwa kukitimiza kutokana na kutoufahamu mwenge huo pamoja na kutojua faida zake kwana tangu nchi hii ipate Uhuru mwenge huo haujawahi jufika katika kijiji hicho hivyo kuwafanya wananchi hao kutoona umuhim wa Mwenge kwao lakini pia kutokana na ubovu wa miundombinu kama barabara pamoja na gharama za usafiri kutoka kijijini hapo mpaka kufika mjini Iringa ziliwalazimu wanachi hao kutochangia michango hiyo.
Aidha mwenyekiti huyo amesema alilazimika kutoa fedha za michango ya shule ili kulipa mchango huo kwani katika kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto pia ya Elimu kwa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishia kama chaki pamoja na vitabu hali ambayo ilichangia kwa kiasi kikubwa mwenyekiti huyo kuto wasilisha michango ya Mwenge baada ya kununua vifaa vya shule ili viwasaidie wanafunzi katika kusoma.
Hasira na kauli kali kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya ilitokana na kupokea taarifa kutoka kwa diwani wa kata ya Udekwa kuwa mwenyekiti huyo anazuia maendeleo ya kijiji kwa kuwazuia wananchi kulipa michango ya maendeleo kitendo ambacho amekanusha nakusema ni uchonganishi na siyo kweli,Hivyo amewataka wananchi kuwapuuza wanasiasa wanaochochea uhasama baina yao na wanaotaka maendeleo yao yarudi nyuma bali waendeleze umoja na mshikamano kama kawaida.
Mwenyekiti wa kijiji cha Udekwa Bw.Obadia Lubugo akizungumza na waandishi wa habari |
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Kilolo Bw.Clay Meshack Mwitura akiongezea maneno katika malalamiko hayo |
No comments:
Post a Comment