Christopher Mwakasege: Summer Conference 2012, UK
Mwalimu
Christopher Mwakasege mnamo tarehe 17-19 August 2012 anatarajia kuwa mnenaji
katika Summer Conference 2012 itakayoyanyika nchini UINGEREZA jimbo la MILTON
KEYNES.
Kongamano hili limeandaliwa na umoja wa Watanzania Wakristo waishio katika bara la Ulaya (CITE).
Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa CITE, Mch Emmanuel Chatawe, CITE SUMMER CONFERENCE 2012 itafanyika katika ukumbi wa Oakgrove Leisure centre Brickhill Street Middleton Milton Keynes MK10 9JQ
Kongamano hili limeandaliwa na umoja wa Watanzania Wakristo waishio katika bara la Ulaya (CITE).
Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa CITE, Mch Emmanuel Chatawe, CITE SUMMER CONFERENCE 2012 itafanyika katika ukumbi wa Oakgrove Leisure centre Brickhill Street Middleton Milton Keynes MK10 9JQ
Tarehe na muda:
17/08/2012 Time 2:00pm-9pm 18/08/2012 Time 10am-9pm 19/08/2012 Time 11am-7am
TOFAUTI
YA ZAKA NA DHABIHU
Kutokutoa zaka na dhabihu ni kumwibia Mungu. Mtu aliye mkristo
asipotoa zaka na dhabihu anaitwa mwizi.
Kuna wakristo ambao ni wezi lakini wao hawajui yakuwa ni wezi.
Wamemwibia Mungu zaka na dhabihu. Mungu anasema hivi:
“Je! mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini
ninyi mnaniibia
mimi. Lakini ninyi mwasema, tumekuibia kwa namna
gani? Mmeniibia ZAKA na DHABIHU” (Malaki 3:8)
Kati
ya amri tulizopewa na Mungu ni kwamba tusiibe. Kuiba ni dhambi. Na
dhambi ina adhabu yake. Popote palipo na dhambi, laana hutokeza. Kwa
wale wanaomwibia Mungu kwa kutokutoa zaka na dhabihu, wamefunikwa na
laana. Ndiyo maana Mungu alisema hivi:
“…..
Mmeniibia Zaka na Dhabihu. Ninyi mmelaaniwa
kwa laana; maana
mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote
(Malaki 3:8b, 9).
Laana
maana yake ni kutokufanikiwa, kutofaulu, kutokustawi, kukosa furaha,
kukosa amani, na kukosa mwelekeo sahihi. Ni wazi kuwa wakristo wengi
hawana furaha, hawana amani na hawafanikiwi katika maisha yao ya kila
siku, kwa sababu hawamtolei Mungu zaka na dhabihu.
Unapokosa kumtolea Mungu ili ujenzi wa nyumba yake – kanisa uendelee,
Hagai 1:6 anatuambia Mungu anasema hivi;
“Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula
lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika
nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata
mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka”.
Zaka
ni kitu gani?
Zaka ni fungu la kumi la pato lako. Hebu isome na kuitafakari mistari
ifuatayo;
“Tena
zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi,
ni ya Bwana, ni takatifu kwa Bwana ….Tena zaka yote ya ng’ombe, au
ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; SEHEMU YA KUMI watakuwa ni
watakatifu kwa Bwana” (Mambo ya Walawi 27:30 –32).
“…Toa
fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo,
uliweke ndani ya malango yako; na Mlawi kwa kuwa hana
fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na
yatima, na
mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako,
na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu
wako, akubarikie katika
kazi yote ya mkono wako
uifanyayo”(Kumbukumbu la Torati
14:28-29).
Zaka
ni fungu la kumi la pato toka mshahara wako ofisini, shambani au
kwenye mifugo. Tena zaka hii ni ya Bwana na ni Takatifu.
Mtu asipoitoa zaka hii anamwibia Mungu. Zaka si yako hustahili kukaa
nayo wala kuitumia nje ya utaratibu wa Mungu.
Lakini Malaki 3:10a anasema; “Leteni zaka
KAMILI ….” Maana yake nini maneno haya? Maana yake ni
hii; ikiwa kwa mfano mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/= (
kabla ya makato) – fungu la kumi au zaka unayotakiwa kutoa ni
shilingi 200/= ambayo ndiyo zaka kamili ya mshahara wako. Ukileta
pungufu yake hiyo si zaka kamili.
Tena kwa mfano umevuna magunia 10 ya mahindi toka shambani mwako –
zaka kamili unayotakiwa kutoa ni gunia moja bila kupungua. Kumbuka
mzaliwa wa kwanza wa mifugo yako ni wa Bwana.
Unaweza ukasema habari za kutoa zaka ni za agano la kale na siyo za
agano jipya.
Waebrania
7:5-10 inatuambia wazi ya kuwa Ibrahimu alitoa fungu la kumi. Kama
Ibrahimu alitoa sehemu ya kumi, Je! si zaidi sana kwetu sisi tulio
uzao wake kwa imani ndani yake Kristo? Maana imeandikwa hivi;
“Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu na
warithi sawasawa na ahadi”
(Wagalitia
3:29). Soma pia Wagalitia 3:13,14).
Dhabihu
ni kitu gani?
Dhabihu
ni matoleo yanayotolewa baada ya kutoa sehemu ya kumi ya pato lako.
Kwa mfano, kama mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/=, basi
sehemu ya kumi (zaka) ni shilingi 200/=. Kiasi cho chote utakachotoa
ju ya shilingi 200/= ndiyo matoleo yako. Kwa mfano ukitoa shilingi
210/= toka kwenye mshahara wako wa shilingi 2000/=, Basi, shilingi
200/= ni zaka; na shilingi 10/= ni dhabihu au matoleo au sadaka ya
kawaida.
Kiasi
utakachotoa katika dhabihu/matoleo, ndicho kitakachokuwa kipimo
kitakachoweka kiwango chako cha kupokea. Imeandikwa hivi:
“Lakini nasema neno hili, APANDAYE HABA
ATAVUNA HABA; APANDAYE KWA UKARIMU ATAVUNA KWA UKARIMU. Kila mtu na
atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa
lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na
Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, MKIWA NA RIZIKI
ZA KILA
NAMNASIKUZOTE,mpatekuzidisanakatikakilatendojema;kamailivyoandikwa,
Ametapanya, amewapa maskini, haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye
mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda
na kuzizidisha, naye ATAYAONGEZA MAZAO YA HAKI YENU, MKITAJIRISHWA
KATIKA VITU VYOTE MPATE KUWA NA UKARIMU WOTE; umpatiao Mungu shukrani
kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii HAUWATIMIZII WATAKATIFU
RIZIKI WALIZOPUNGUKIWA TU, Bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani
nyingi apewazo Mungu; kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo,
WANAMTUKUZA MUNGU kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya
Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote”
(2Wakorintho 9:6-13)
Soma
tena mistari hiyo hapo juu, lakini sasa tafakari zaidi maneno
niliyoyaandika kwa herufi kubwa. Utaona kuwa usipokuwa mwaminifu
katika utoaji, wewe mwenyewe unakosa kufanikiwa, na pia unamkosesha
Mungu shukrani na utukufu ambao angepata kwa utoaji wako.
Zaka
na dhabihu zitolewe wapi?
Hili
jambo linahitaji uongozi wa Roho Mtakatifu, ili upate ufahamu Mungu
anataka upeleke wapi zaka na matoleo uliyo nayo.
Hili ni muhimu kwa kuwa Biblia inazungumza juu ya kupeleka kanisani (Malaki 3:10-11), kwa watakatifu (2Wakorintho 9:12), kwa maskini (2Wakorintho 9:8-9), kwa watumishi wa Mungu (1Wafalme 17:10-24; 1Wakorintho 9:7-14); kwa wajane, - na kadhalika.
Muombe Mungu akuongoze mahali pa kupeleka. Amani ya Kristo na iamue
moyoni mwako.
Baraka
Tele!
Kuna
baraka tele za mafanikio kwa mkristo aliye mwaminifu katika kumtolea
Mungu zaka na matoleo.
Katika
Malaki 3:10 imeandikwa hivi; “Leteni
zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu,
mkanijaribu kwa njia hiyo (YA UTOAJI) asema Bwana wa Majeshi; mjue
kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na KUWAMWAGIENI BARAKA,
HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA AU LA”.
Je!
umewahi kukutana na mkristo ambaye anashuhudia kuwa Mungu amempa
baraka nyingi hata HANA MAHALI PA KUZIWEKA? Ni wazi kuwa ahadi hii
haijatimia kwa kuwa hatujawa watendaji na Neno kikamilifu katika
utoaji.
Soma mistari hii hapa chini uone baraka zingine zinazotokana na utoaji;
“Azaria Kuhani Mkuu, wa nyumba ya Sadoki,
akamjibu,
akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo
nyumbani
kwa Bwana, tumekula na KUSHIBA
NA KUSAZA TELE;
kwa kuwa
Bwana amewabariki watu wake; na kilichosalia
ndiyo
akiba hii kubwa. Ndiko Hezekia akaamuru kutengeneza vyumba nyumbani
mwa Bwana;
wakavitengeneza. Wakayaingiza MATOLEO na ZAKA
na vitu
vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu ….”
(2Mambo ya Nyakati 31:10-12).
Kwa
nini wakristo wengine wanapungukiwa vyakula, wakati tuna nafasi ya
kumruhusu Mungu kutubariki kwa vyakula tele? Mpe Mungu nafasi ya
kukubariki kwa kumtolea zaka na matoleo!
Anza
Sasa!
Nakushauri ya kuwa kama ulikuwa hutoi sehemu ya kumi au zaka pamoja na
matoleo ya kutosha – anza sasa.
Jambo la kwanza, kumbuka kutubu kwa Mungu katika Jina la Yesu Kristo
kwa kuwa ulimwibia zaka na dhabihu kwa kutokumtolea.
Halafu
mwombe Mungu akuwezeshe kusimama katika uaminifu wa kumtolea zaka na
dhabihu ili apate nafasi ya kukubariki zaidi kama tulivyoona, na kama
alivyoahidi. |
Mawasiliano zaidi:
Rev. Chatawe 07944632826 Pas. Kimani 07522050673 Sis Jane 07522302935 Sis. Flora 07916160641 |
No comments:
Post a Comment