WADAU WAKISHIRIKIANA KWA PAMOJA UJANGILI WA MENO YA TEMBO UTAKOMA
Wadau wa mazingira na udhibiti wa meno ya Tembo nyanda za juu kusini |
Wadau wa sekta ya maliasili na utalii mikoa ya nyanda za
juu za juu kusini wametakiwa kushiriki ipasavyo katika jitihada za pamoja
katika kukabiliana na tatizo la majangili wa wanyama katika maeneo yanayopakana
na hifadhi za taifa.
Maadhimio hayo yametolewa katika semina ya wadau wa
ulinzi wa maliasili juu ya wimbi la ujangili wa tembo nyanda za juu kusini
baada ya wadau hao kuonesha nia ya pamoja katika kuhakikisha wanapambana kwa
kushirikiana na vyombo vya usalama katika maeneo hayo kudhibiti vitendo hivyo
ambapo kila mwaka zaidi ya tembo elfu 10 huuwa.
Semina hiyo iliyoandaliwa na mradi wa kuboresha usimamizi
na uhifadhi wa mazingira, Strengthening the Protected Area Network in
Southern Tanzania SPANSET imelenga kujadili jitihada za makusudi za wadau
hao wakiwemo ofisi za wakuu wa mikoa Iringa,Mbeya,Njombe na Dodoma pamoja na
asasi mbalimbali zikiwemo Interpol Tanzania,Interpol Kenya,Cites/Mike
Tanzania,Trafic Tanzania na wadau wengine wa maliasili na utalii ambao
wanalenga kukabiliana na tatizo hilo la ujangili wa wanyama hususani tembo.
Katika semina hiyo imebaini kuwepo kwa changamoto nyingi
zinazo ikabili sekta ya maliasili na utalii hapa nchini na kuathiri kwa kiasi
kikubwa Rasilimali wanyama ambapo baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kuwepo
kwa kundi kubwa la wahamiaji haramu katika misitu iliyo karibu na mbuga,kuzagaa
kwa silaha zinazoletwa na wageni kutoka nchi za jirani ambazo zina migogoro ya
kisiasa,kukua na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu hususani kilimo pamoja
na kushamili kwa biashara haramu ya nyara za serikali zikiwemo meno ya tembo,pembe za faru pamoja
na ngozi za wanyama mbalimbali.
Hivyo wadau hao wameishauri serikali pamoja na wananchi
kushirikiana kwa pamoja katika kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika pindi
wanapoona matukio ya kijangili yanajitokeza kwani wanao husika na vitendo hivyo
wapo katika jamii.
Kwa upande wake profesa Mutayoba wa chuo kikuu SUA mkoani
morogoro ambaye ndiye mmoja wa watafiti wa DNA nchini ameshauri kutumia vipimo
kupima pembe hizo kitaalamu ilikubaini mahali zinapotoka ili kuongeza udhibi
No comments:
Post a Comment