MASHINE ZA KUTOLEA LISITI (EFDs) KAZI BADO IRINGA WATAKIWA KUTEKELEZA AGIZO LA SERIKALI
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Iringa, Rosalia Mwenda akizungumza na mtandao huu |
Wafanyabiashara mkoani iringa wametakiwa kutumia
elimu wanayoipata kupitia semina mbalimbali zinazotolewa na mamlaka ya mapato
Tanzania TRA ili waweze kufaham zaidi matakwa ya sheria.
Rai hiyo imetolewa na meneja wa mamlaka hiyo mkoani
Iringa Bi Rosali mwenda wakati akizungumza na Overcomers redio ofisini kwake
hii leo kuhusiana na mwenendo mzima wa
utumiaji wa mashine za kielectronic kwaajili ya kutolea lisiti kwa wateja
(EFDs)
ambapo amesema kuwa zoezi hilo linaendelea kuwepo
kwa mujibu wa sheria kwani hakuna mtu wala kikundi cha watu walioamua kuwepo
kwa mashine hizo bali ni uamuzi wa serikali ili kudhibiti na kurahisisha
ukusaji wa mapato nchini.
Hivyo amewataka wafanyabiashara mkoani hapa kutambua
kuwa suala la kutumia mashine hizo ni la kisheria pia wanatakiwa kulichukulia
uzito kwani kupuuzia zoezi hilo ni ukiukwaji wa sheria iliyowekwa na mamlaka
husika.
Aidha Bi Mwenda amesema wafanyabiashara watambue
kuwa awamu ya kwanza ya utumiaji wa mashine hizo umekamilika uliokuwa
ukiwahusisha wale walio na mtaji wa kuanzia zaidi ya million 40
na sasa wameanza awamu nyingine inayohusisha wale wenye mtaji wa kuanzia
milioni 14 hadi 39 na itaendelea hadi itakapofika kwa wafanyabiashara wote.
Akielezea juu ya mahusiano ya mamlaka hiyo na
wafanyabiashara Bi Mwenda amesema kwasasa hakuna tatizo lolote kati yao na
mpaka sasa wameanza kuwapelekea barua za kuwakumbusha wafanyabiashara
wanaotakiwa kuwa na mashine hizo.
Ajali yaua Mmoja Iringa
Mtu mmoja ameripotiwa kufariki dunia mkoani Iringa
kwa ajali ya gari.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Iringa
Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa ajali
hiyo imelihusisha gari dogo aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 142
CRA lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Dodoma.
Kamanda Mungi amesema ajali hiyo imetokea mnamo
tarehe 10.03.2014 majira ya saa 11:00 jiaoni katika eneo la Igingilanyi wilaya
ya Iringa vijijini ambapo amemtaja
dereva wa Gari hilo kuwa ni Darton Ilomo(22) mwanafunzi wa Chuo cha UCC
Kilichopo jijini Dar es salam
Aidha amemtaja aliyefariki kutokana na ajali hiyo
kuwa ni Rose Mwakabuku (55) muuguzi katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambaye
pia ni mkazi wa mwembetogwa katika manispaa ya Iringa mjini na amesema marehemu
amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospital ya mkoa wa Iringa, huku
chanzo cha ajali hiyo kikiripotiwa kuwa ni mwandokasi hivyo Mungi amewataka
madereva kuwa wastaarabu pindi wanapoendesha vyombo vya moto.
No comments:
Post a Comment