Tuesday, February 21, 2012

WANANCHI IRINGA WAILILIA IRUWASA
Wananchi katika manispa ya Iringa wameiomba idara ya maji(IRUWASA) mkoani hapa kuboresha miundombinu ya maji iliyoharibika na kusababisha uvujaji wa maji kiholela katika maeneo mengi ya manispaa hiyo.

Wakizungumza na Mtandao huu wananchi hao wameonesha kusikitishwa kwao na tatizo la uvujaji wa maji kiholela jambo ambalo limekuwa likisababisha kukosekana kwa huduma hiyo katika maeneo yao ambapo wameyataja maeneo yaliyo athiriwa na uvujaji wa maji hayo kuwa nia pamoja na Mlandege,Flelimo,Mwangata na maeneo ya mshindo.

Wamesema kuwa kutokana na uvujaji huo unachangi kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa miundo mbinu kama barabara na maeneo ya makazi ya watu hivyo wameuomba uongozi wa idara hiyo kulishughulikia ili kupunguza kero hiyo.

Kwa upande wake afisa mahusiano wa idara ya maji manispaa ya iringa bi Restuta Sakila alipohojiwa na mtandao huu ili kulizungumzia tatizo hilo amekili kuwepo kwa tatizo hilo ambalo amesema tayari wameiweka mikakati maalum kwaajili ya kurekebisha tatizo hilo,ambapo mpango huo utaanza kushughulikiwa mapema mwezi huu kwa kuwa tayari kila kitu kipo tayari

Hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa karibu na idara hiyo pale wanapoona tatizo ambalo ni kubwa kutoa taarifa ili liweze kushughulikiwa mapema iwezekanavyo kupunguza uharibifu huo.Pia amewataka wananchi kuto watumia mafundi wanaochangisha fedha za matengezo nje ya ofisi ili kupunguza kero hizo.   

No comments:

Post a Comment