FEBRUARY 21/2012
Chama cha watu wenye ulemavu manispaa ya Iringa mjini,
kimeyataka mashirika binafsi yanayoomba miradi ya kusaidia watu wasiojiweza
kupitia barua za maombi yao
na kuhakikisha wanatekeleza yale waliyo yaandika katika barua hizo.
Akizungumza na mtandao, katibu wa chama hicho manispaa
ya Iringa bwana Haruna Mbata amesema tayari wamebaini kuwa kuna baadhi ya
mashirika ambayo yaliomba yapewe fedha za kuwasaidia watu wasio jiweza wakiwemo
wajane,walemavu,watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu baada ya
kupokea fedha hizo matokeo yake hujinufaisha wenyewe.
Aidha bwana mbata amesema, kutoka na vitendo
vinavyofanywa na baadhi ya mashirika hayo ya kutotekeleza majukumu yao
kimewafanya waweze kutengeza mikakati maalum kwaajili ya kukagua nyaraka zote
zilizoandikwa ili kuona ikiwa wanatekeleza ipasavyo, pindi itakapobainika kuwa
kuna ubadhirifu ifikapo mwezi wa kumi na mbili mwaka huu, amesema watatakiwa kufuta yale waliyoyaandika katika
miongozo hiyo.
Hivyo amewataka wale wanaosimamia miradi hiyo
kutekeleza yale waliyoyandika kwa kuwasaidia watu wasiojiweza kuliko
kujinufaisha wenyewe kwani kufanya hivyo nikosa kwamujibu wa usajili wa miradi hiyo
FEBRUARY 21/2012
S
No comments:
Post a Comment