Friday, February 24, 2012

Afisa mnajimu wa jeshi la polisi mkoa Iringa
Bundara Msiba

               
      Polisi jamii Iringa kupewa kipaombele ili kutokomeza uharifu

Wananchi mkoani Iringa wameaswa kutoa ushirikiano wa karibu kwa jeshi la polisi ili kutokomeza uharifu katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na Afisa mnajimu wa jeshi la polisi mkoani hapa bwana Bundara Musiba wakati wa mahojiano maalum na mtandao huu juu ya njia za kutokomeza uharifu pamoja na Polisi jamii katika mkoa wa Iringa ambapo amesema wananchi wanao wajibu wa kuhakikisha wanatoa taarifa ya uharifu pindi unapo jitokeza katika maeneo yao.

Amesema suala la polisi jamii ni la msingi kwani linaweza kusaidia jeshi la polisi kutambua maeneo ambayo kunatokea uharifu pia kuwatambua watu wanaojihusisha na vitendo vya uharifu,hii imekuja kutokana na matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika mkoa wa iringa yakiwemo ya watu kujinyonga na pia kuuawa kwani kuliachia jeshi la polisi pekee haliwezi bali wanahitaji nguvu zaidi kutoka kwa wananchi kwani ndiyo wanaoishi karibu na waharifu hao.

Aidha ameshauri jamii kuacha vitendo vya kuchukua sheria mkononi pindi wanapo mkamata muharifu na badala yake wamfikishe katika kituo cha polisi kwani kufanya hivyo kunaweza kusaidia jeshi la polisi kuwakamata waharifu wengine baada ya mahojiano na mtuhumiwa kwani anaweza kuwataja waharifu walio shirikiana katika kufanya uharifu.

No comments:

Post a Comment