Naibu waziri wa Maji jana ameendelea na ziara katika jimbo lake la Njombe Magharibi.
Naibu waziri wa maji ambaye pia ni
mbunge wa jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge jana ameendelea na
ziara yake kuwatembelea wananchi wa Jimbo hilo ikiwa kwa siku ya jana
amezungukia tarafa ya Imalinyi na kuzungumza na wananchi wa kata za Ulembwe na
Imalinyi
Mhandisi Lwenge jana amezungukia vijiji vitatu na kuzungumza na wananchi hao huku akiwa katika kijiji cha Ulembwe amewataka wananchi kuonesha ushirikiano mkubwa katika kukuza maendeleo.
Aidha amewapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa kujenga ofisi ya kata kwa kutumia fedha aliyo itoa katika kipindi cha nyuma kiasi cha shilingi milioni mbili na laki sita kwani mpaka sasa ofisi hiyo imebakia hatua ya kupaua.
Usalule ni moja ya kijiji kilicho tembelewa na mbunge Lwenge ambacho kimemfurahisha kutokana na jitihada kubwa za kimaendeleo yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na kufanikisha ujenzi wa jiko na choo cha kisasa kwa ajili ya zahanati ya kijiji hicho.
Akisoma taarifa ya kijiji hicho cha Usalule kaimu afisa mtendaji wa kijiji bwana Elias Chatanda amesema kuwa licha ya mafanikio hayo yote lakini pia tayari wamesha nunua tofali elfu kumi kwaajili ya ujenzi wa nyumba moja ya mwalimu katika shule ya msingi Usalule.
Akiwa katika kijiji cha mwisho kwa siku ya jana ambacho ni kijiji cha Igodivaha kilichopo kata ya Imalinyi wananchi wengi wamelalamikia kitendo cha serikali kushindwa kuwafikishia mbolea za ruzuku huku wazee wengi ambao ndio walengwa wa zoezi hilo kukosa pembejeo hizo.
Ziara hiyo kwa siku ya leo inaendelea katika kata ya Mdandu kwa kuanzia kijiji cha Sakalenga kikifuatia kijiji cha Ihanja na kumalizika katika kijiji cha Itambo.

No comments:
Post a Comment