SPIKA MAKINDA ATOLEA UFAFANUZI KUHUSU MKOA MPYA WA NJOMBE
Speaker wa Bunge la Jamhuri
ya muungano wa Tanzania ambaye ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini Bi.Anne
Makinda jana ameweza kutolea ufafanuzi juu ya kuanza kwa mkoa mpya wa Njombe
huku akisema suala hilo ni la kuvuta subira kwani maandalizi yamesha fanyika
hivyo kilichobaki ni kusubiri tamko la Rais kumtangaza mkuu wa mkoa.Aidha Bi.Makinda amewataka wananchi wa mkoa mpya wa Njombe kutumia nguvu zao na fursa za ujasiliamali walizo nazo katika kujikwamua na hali ngumu ya umasiniki kupitia kuanza kwa madini ya Liganga na mchuchuma yaliyopo Wilayani Ludewa kwani mara baada ya kuanza kwa zoezi hilo kutakua na mwingiliano wa kibiashara.
Aidha mbunge huyo jana ameweza kuahidi kutoa mifuko 100 ya cement ili kukamilisha ukarabati wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Joshoni katika kata ya Mjimwema mjini hapa.
Katika hatua nyingine ameelezea sababu za vurugu bungeni na kusema bunge la awamu hii lina vijana wengi na wengi wao hawafahamu sheria za bunge.
Hata wananchi waliweza kuuliza maswali ambayo majibu yake alianza mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe bwana Edwin Mwanzinga na kusababisha kusambalatika kwa wananchi hao kwenye mkutano wa Spika wa bunge akiwa kwenye ziara ya jimbo lake kutokana na majibu yake akiwa eneo la NATIONAL HOUSING mjini njombe.
Kusambalatika kwa wananchi hao kumetokana na baadhi ya majibu ya mwenyekiti wa halmashauri ya mji huo zikiwemo hoja za mbolea za Ruzuku pamoja na kuhamishwa kwa madera wa stendi ya malori iliyopo katika eneo la National Housing mjini Njombe.
Ziara hiyo kwa siku ya jana ilianzia katika kata ya Mjimwema hususani kwa kuanzia katika mtaa wa Joshoni ambako ameahidi kutoa mifuko 100 ya cement kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa ofisi ya serikali ya mtaa huo ikiwa leo anaendelea na ziara yake
No comments:
Post a Comment