Tuesday, June 5, 2012

Hii ndiyo gari ilyopa ajali mkoani mbeya nakusababisha vifo vya watu 13 na wengine 20 kujeruhiwa
Hayati mzee Mathius Kihaule

 Aliyekuwa mbunge wa Ludewa, mzee Mathias Kihaule amefariki jana saa tisa na nusu alasiri, katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, ambako alikuwa amelazwa kutokana na maradhi ya ugonjwa wa moyo. Mzee Kihaule alikuwa ni mbunge wa Ludewa toka mwaka 1980 - 1985, 1985 - 1990, na 1990 - 1995.

 

Mzee Kihaule ambaye aliyewahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliwahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.

 

Kabla ya mauti, mzee Kihaule alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Lugarawa, ambako pia alikuwa akijishughulisha na shughuli za Kilimo. Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda kijijini kwake Lugarawa, LudewaHabari na

No comments:

Post a Comment