 |
Mhanga wa tukio la ajali ya moto Bi Jojina Kahemela akitahamaki kilicho sababisha kuunguliwa na nyumba |
 |
Mwenyekiti wa mtaa wa Frelimo C Bwana Geoge Mwanjombe akishuhudia tukio |
 |
Hii ni nyumba iliyoathiriwa na ajali ya moto ikionekana kwa nje imeathiriwa ndani |
 |
Wananchi wa Frelimo C wakisaidia kuokoa mali zilizo nusulika wakati wa tukio |
 |
Baadhi ya wakazi wa Frelimo C wakishuhudia ajali ya moto ilivyotokea |
 |
Mwandishi IMTV Ibrahim Kitan'gara akishuhudia tukio la moto |
 |
Baadhi ya vyombo vilivyo nusulika katika ajili ya moto na kuokolewa na wasamlia wema wa mtaa wa frelimo |
 |
Gari ya zima moto ikisaidia kuzima moto katika mtaa wa frelimo |
Nyumba moja katika mtaa wa Frelimo C kata ya kwakilosa
manispaa ya Iringa mjini imenusurika kuteketea baada ya kutokea kwa hitlafu ya
umeme na kusababisha moto ulio unguza baadhi ya mali za nyumba hiyo.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja na nusu za asubuhi
hali ambayo imewashangaza wengi hususani wananchi wa maeneo hayo walioshiriki
kuokoa baadhi ya mali
zilizokuwemo katika nyumba hiyo na jitihada hizo kuweza kuzaa matunda na
kufanikiwa kuzima moto huo.
Akizungumzia juu ya ajali hiyo mmiliki wa nyumba hiyo Bi
Jojina Kahemela amesema chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyojitokeza
ambayo imeanzia katika chumba chake ambako ndiko walilala watoto japo anasema
anashindwa kutambu chanzo cha hitlafu hiyo,hivyo amewaomba wananchi wenye
mapenzi mema kumsaidia baadhi ya vitu vilivyo haribiwa na moto huo ikiwemo
magodoro,vyombo mbalimbali pia amewashukuru wananchi waliojitokeza kumsaidia
kuzima moto huo bila nguvu ya zima moto ya manispaa ambao waliwasili katika
tukio hilo na kukuta hali imetulia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Bw Geoge Mwanjombe
amewapongeza wananchi wa mtaa wake kwa ushirikiano walio uonesha katika
kusaidia kuzima moto huo ambao usinge shughulikiwa mapema ungeweza ksababisha
madha makubwa zaidi nao mashuda wa tukio hilo wamezungumzia tukio hilo kuwa
limewashtua lakini wametoa tahadhari kwa jamii kuwa makini na matumizi ya umeme
ili kuepusha matukio ya ajali yatokanayo na umeme.
No comments:
Post a Comment