Kaya 55 zilizopo Wilayani Magu, mkoa wa Mwanza hazina mahali pa kuishi
baada ya nyumba zao zaidi ya 90 kubomolewa kisha kuchomwa ikiwa ni
sehemu ya kutimiza amri ya Serikali nyumba hizo kubomolewa kupisha eneo
hilo linalotajwa kuwa ni Hifadhi ya Taifa.
Tukio hilo linadaiwa
kufanyika kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Agosti 2 mwaka huu, ambapo zoezi
hilo liliendeshwa chini ya usimamizi wa Mkuu Mpya wa wilaya hiyo
Jacquline Liana, akishirikiana na Jeshi la polisi Wilayani humo.
No comments:
Post a Comment