Wednesday, August 1, 2012


MWIMBAJI WA THE VOICE ANAENDELEA VIZURI, KURUDI HOSPITALI HII LEO

Obed akiwa na Pastor Paul Safari wa DPC alipomtembelea nyumbani kumjulia hali.
                 
Mwimbaji wa kundi la The Voice la nchini bwana Obed John Mark ambaye alipata ajali jumatano iliyopita maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam, hali yake inaendelea vizuri ambapo asubuhi ya leo anatarajia kuelekea hospitali ya rufaa ya Muhimbili kwa ajili ya uchukuaji wa kipimo cha T scan.

Akizungumza na GK, Obed amesema anamshukuru Mungu anaendelea vizuri kwasasa ingawa bado anasikia maumivu kwenye shingo licha ya kutumia dawa alizopatiwa na daktari Julius Dinda. Aidha mwimbaji huyo amesema ametoa shukrani zake kwa watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifika nyumbani kwao kumjulia hali kitendo ambacho amesema amefarijika sana kuona kuna watu wanamjali.

Mwimbaji huyo alipata ajali maeneo ya Sinza Kamanyola wakati akielekea Magomeni, ambapo alirushwa hadi mtaroni na kuumia sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mikono na miguu na hali yake kuelezwa kuwa haikuwa nzuri.Aidha kwa upande wa kundi hilo wakitoa taarifa za maendeleo ya mwimbaji huyo siku chache zilizopita wamesema;-


The Voice.

 

JIUNGE NA AGUSTINO KIHOMBO, NDANI YA OVERCOMERS FM  RADIO  

Jiunge na Agustino Kihombo a.k.a A 2 K nadai ya Redio ya washindi Overcomers fm Redio 98.6 kila siku za wiki kuanzia saa 07:00 hadi saa 09:30 asubuhi katika kipindi cha tujadili jumatatu hadi Ijumaa lakini pia katika kipind cha Michezo na Burudani saa MOJA JIONO hadi saa MBILI kamili usiku.

Pia siku ya jumamosi katika kipindi cha MIZANI kili jumamosi kuanzia saa 02:00 mchana hadi saa 04:00 jioni katika mahojiano na ufafanuzi wa mada za kijamii,kisiasa na kiuchumi pamoja na Uchambuzi wa michezo.

No comments:

Post a Comment