Rais Kikwete Akutana Na Dkt. Asha Rose Migiro
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Dkt.Asha Rose Migiro ikulu jijini Dar es
Salaam leo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Dkt.Asha Rose Migiro ikulu
jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja
wa Mataifa Dkt.Asha Rose Migiro ikulu jijini Dar es Salaam leo. Chanzo:
Freddy Maro
Mabasi ya Dar Express, Simba Mtoto yamegongana uso kwa uso eneo la Wami
Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na basi la Simba Mtoto lililokuwa linaenda Tanga yamegongana uso kwa uso maeneo ya Wami. Mwanahabari wa "Globu ya Jamii" aliyekuwa eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna maafa ya watu kupoteza uhai yaliyoropotiwa ila, watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado hakijafahamika.Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Chalinze.
Maiti Mv Skagit zafikia 89
Idadi ya maiti
za ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Skagit zimeongezeka na kufikia 89
baada ya miili mingine 11 kupatikana leo katika maeneo manne tofauti ya
visiwa vidogovidogo vilivypo mwambao wa Zanzibar.
Afisa Habari
Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa
miili iliyopatikana leo, sita ni wanaume akiwemo kijana mdogo na mingine
mitatu ya wanawake.
Inspekta Mhina
amesema, maiti zote zimezikwa katika makaburi ya pamoja ya Kama yaliyopo
nje kidogo ya mji wa Zanzibar chini ya usimamizi wa Jeshi la la
Wananchi wa Tanzanaia JWTZ, Jeshi la Polisi, MKMK, JKU na Varantia.
Amesema miili
hiyo ilipatikana katika viisiwa vya Pungume, Fumba, Chumbe na eneo
linalokupwa na kujaa maji la Funguyasini maeneo jirani na kisiwa mama
cha Unguja.
Naye Mkuu wa
Polisi Kikosi cha Wanamaji na Bandari Zanzibar SP Martin Lisu, amesema
kuwa kunauwezekano mkubwa kuwa maiti hizo zinaibuka kutoka katika meli
hiyo ya Skagit.
Kamanda Lisu,
amesema kuwa kutokana na kuendelea kuibuka kwa maiti hizo, Maafisa wa
vyombo vya Ulinzi na Usalama wanaendelea na zoezi lao la kutafuta miili
mingine na kupokea taarifa za kuonekana kwa mwili kutoka kwa watu wenye
vyombo binafsi vya uvuvi na kuzifuatilia.
Hivi karibuni
akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete,
Daktari Mkuu Mwelekezi wa Jeshi la Polisi nchini Dk. Ahamed Makata,
alisema kuwa maiti nyungi zitaweza kupatikana ifikapo siku ya nne tangu
kuzama kwa meli hiyo.
Alisema tabia ya
maiti ya binadamu aliyekufa maji na kuzama, haiwezi kukaa chini ya maji
kwa muda mrefu kama haikufungwa na kitu kizito kabla ya kuzama.
"Kwa kawaida
maiti ya mtu aliyekufa maji haiwezi kukaa ndani ya maji wakati wote na
kwamba hata kama itaendelea kubaki majini lakini katika muda wa kuanzia
siku tatu na nne mwili ama miili hiyo nilazima ianze kuibuka na kuelea
juu ya maji". Alisema Dk. Makata.
No comments:
Post a Comment