Sunday, July 22, 2012




 Magazetini Jumapili Hii july 22,2012











TATIZO LA MAJI LAWA KERO KWA WANANCHI WA NDULI MANISPAA YA IRINGA MJINI,AHADI ZA SERIKALI BUBU BAADA YA UCHAGUZI ZAWAACHA SOLEMBA BILI KUJUA CHA KUFANYA
Mwananchi wa Nduli akuzungumzia tatizo la maji Nduli


Mkazi wa Nduli katika huzuni ya kukosa maji Nduli
Mchoma nyama za mbuzi katika n=misitu ya katika kata ya kising'a Ismani Iringa

UGOMVI ULIOKUWA UKIHUSISHA PANDE MBILI ZA FAMILIA YA MAREHEMU WASULUHISHWA MKOANI MBEYA,.


 Sehemu ya mabati 57 yaliyotolewa na Familia ya Mligula iliyokuwa ikigombea mali za marehemu Eva Emmanual Mligula na Emmanuel Mwaigaga na kutoa vitisho kwa njia ya mtandao kwa Bwana Allan Mwaigaga,ambaye aliitaka familia hiyo kuchangia maendeleo ya Shule tatu za Msingi ya Itewe,Pankumbi na Mwashoma.
Viongozi wa kikabila(Machifu) na wanafamilia wa pande zote mbili za marehemu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza tofauti zao.(Picha na Ezekiel Kamanga)
*******
Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Ugomvi wa kugombea mali za marehemu uliokuwa unahusisha familia mbili za marehemu Eva Emmanuel Mligula(38) na Emmanuel Mwaigaga aliyefariki miaka nane iliyopita waliokuwa wakiishi Mtaa wa Utukuyu,Kata ya Uyole Jijini Mbeya umesuluhishwa baada ya familia hizo kukutanishwa na uongozi wa kimila na Serikali.
Awali ugomvi ulianza Julai 13 mwaka huu katika mazishi ya Mjane Eva,kufuatia Baba na kaka wa marehemu huyo kuwazuia ukoo wa Mwaigaga(kiumeni) kutokuwepo katika msiba na kutohudhuria mazishi kwa kile kilichodaiwa kuwa ukoo unaweza kuuza nyumba ya marehemu.
Mvutano huo ulielekea ukoo wa marehemu kubeba kila kitu kilichokuwemo ndani zikiwemo samani kwa kutumia gari yenye nambari T 788 BLK aina ya Fuso na T 314 AVA aina ya Center na kusababisha Bwana Allan Mwaigaga(Mwaji Group) kutoka ukoo unaotuhumiwa kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Uyole.
 Mkuu wa kituo hicho cha polisi Lazaro Kiyeyeu alifika eneo la tukio na kushuhudia vyombo vikibebwa na ukoo wa Mligula naye kwa kushirikiana  na Mwenyekiti wa mtaa Bwana Michael Mwamahondya kuchukua jukumu la kumtaarifu Diwani wa kata ya Uyole Bwana Ngambi Ngela ambaye aliwasihi wananchi waliokuwepo msibani hapo kurudi makwao na hivyo na kila familia ya marehemu kwenda kulilia msiba nyumbani kwao na nyumba hiyo ya marehemu kufungwa na yeye kukabidhiwa funguo kukabidhiwa Bwana Mwaigaga.
Aidha .baada ya funguo hizo kukabidhiwa hali ikawa tofauti kutokana na ukoo wa Mligula kuporomosha matusi na vitisho kwa Bwana Mwaigaga,ambaye alitoa taarifa Polisi na kufunguliwa kesi mbili dhidi ya ukoo huo,ambapo kesi ya kwanza yenye nambari MB/IR/57/67/2012  ya kutishia kuua kupitia njia ya mtandao na kesi ya pili ya Jinai 551/2012 ya kutoa kashifa mbele ya umma na kupora mali za marehemu.
Mnamo Julai 19,mwaka huu Katibu wa mila wa kabila la Kisafwa Chifu Mwalwego alipokea ombi la msamaha kutoka kwa familia ya Mligula kuomba wapatanishwe na ukoo wa Mwaigaga,baada ya kugundua wamefanya makosa ya kuchukua mali za marehemu badala ya kuziacha katika nyumba hiyo ambapo marehemu wameacha watoto watatu wawili wa kiume na mmoja wa kike ambao walipaswa kuacha mali hizo.
 Baada ya kupokea ombi hilo Chifu huyo aliwasiliana na Bwana Mwaigaga ambaye alikubali kusamehe na kutaka akutanishwe na ukoo huo Julai 21 mwaka huu majira ya saa nne katika eneo la nyumba ya marehemu iliyopo mtaa wa Utukuyu na kwamba yeye hataki kulipwa fidia yoyote licha ya kudharirishwa lakini ameutaka ukoo huo uchangie maendeleo katika shule tatu za msingi zinazozunguka eneo hilo ambazo ni Shule ya Msingi Itewe ipewe mabati 19 ya gauge 30 na shilingi 100,000 kwa Chifu wa mtaa huo.
Ameongeza kuwa Shule ya Msingi Pankumbi ipewe mabati 19 na shilingi 100,000 kwa chifu wa eneo hilo na Shule ya msingi Mwashoma ipewe mabati 19 na  shilingi 100,000 na Chifu Mwanshinga apewe shilingi 200,000 kama msuluhishi wa mgogoro huo.
Hata hivyo Julai 21 mwaka huu ukoo wa Mligula,ulilipa shilingi 500,000 na mabati 57 mbele ya uongozi wa Machifu na uongozi wa Kata ya Uyole baada ya kukutanishwa na ukoo wa Mwaigaga.
Kwa upande wake Bwana Allan Mwaigaga alisema hana kinyongo na kuahidi kufuta kesi mahakamani lakini pande zote mbili za familia zishirikiane kuwalea watoto hao walioachwa na marehemu,pia mali zituzwe na nyumba ipangishwe ili pesa zitumike kwa ajili ya kuwasomesha watoto kwani kwa kufanya hivyo iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia za kuhodhi mali za marehemu na kuacha watoto wakihangaika.

TUKIO LA WANAFAMILIA KUGOMBANIA MALI ZA MAREHEMU.

Sehemu ya samani iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu Eva Emmanuel Mligula na Emmanuel Mwaigaga,iliyogombaniwa na ndugu zikiwa zimetolewa nje kwa lengo la kuhamishwa katika Mtaa wa Utukuyu,Kata ya Uyole Jijini Mbeya.
 Baba Mzazi na Kaka wa marehemu Eva wakiwa nje ya nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na  marehemu Eva Emmanuel Mligula na Emmanuel Mwaigaga katika Mtaa huo nayo iliingizwa katika mgogoro wa kugombaniwa,hali iliyopelekea Serikali kuingilia kati..
 Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia tukio la kutolewa kwa vyombo vya marehemu vilivyokuwa vikigombaniwa na wanandugu.
 Mama mzazi wa marehemu Eva,anayefahamika kwa jina la Bi. Magreth Mzegeza(70) aliyevalia nguo nyeupe akiwa na baadhi ya waombolezaji.
 Moja ya magari yaliyotumika kuhamishia shehena ya mali za marehemu.
Sehemu ya Sebule ikiwa tupu baada ya vyombo vyote kubebwa na Kijana huyu alikuwa mstari wa mbele katika kuvitoa vyombo vya marehemu.(Picha na Ezekiel Kamanga,Mbeya).

No comments:

Post a Comment