Ikiwa Serikali itazungumzia kilimo kwanza halafu tukawekeza katika maeneo yenye mti kama hii tutapata kitu
Miti hii kwa mikoa ya nyanda za juukusini hutumika kama zao la kinywaji kinacho tambulika kwa jina la Ulanzi ambacho ndicho kinywaji na kilevi kinachopendwa na watu wengi si wazee wala vijana wa mikoa hii ya nyanda za juu kusini
Inasadikika Ili ukosane na wakazi wa maeneo hayo jaribu kumshawishi akate miti hii na aache shughuli za ugemaji wa kinywaji hicho ambacho ndicho kinacho sababisha uvivu katika jamii za mikoa hiyo ambao hutumia muda mwingi kujihusisha na ugemaji na unywaji wa kinywaji hiki hususani muda wa kazi,kama hiyo haitoshi miti hii inaathari kwa mazao ya chakula kama mahindi kutokana na chumvichumvi inayotokana na mimea hii,
jamii nyingi za Ukanda huu huchanganya miti hii na mazao hali ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa chakula katika maeneo yanayolimwa mianzi hii,
Je,tuwashauri nini ndugu zetu hawa wanaoumia kwa njaa na kupoteza muda mwingi kwa kukaa na kupoteza muda kwa ulevi?
''angalia picha ya mazao ya mahindi na mihogo hapo chini...............
Mianzi mti wa Ulanzi |
Hii ni sehemu ya mji wa Ipogolo Manispaa ya Iringa Mjini |
Serikali ya Tanzania inamtafuta nyoka wake mwenye umri wa miaka 209
Serikali
imedhamiria kumsaka nyoka mwenye umri wa miaka 209 aliyepo katika Msitu
wa Akiba Minziro, uliopo Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera.
Lengo la kumsaka nyoka huyo ni kutokana na ukongwe wake hivyo kuwa kivutio kikubwa duniani hasa katika sekta ya utalii.
Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki nchini, Dkt. Felician Kilahama, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari. Akasema nyoka huyo mwenye futi 47, atapatikana baada ya mapito yake katika msitu huo kuonekana ila ni vigumu kuonekana hadharani kwa sababu hupendelea kuishi mapangoni, “Huyu nyoka lazima tumfanyie mahesabu ya kumkamata kirahisi, umri wa miaka 209 sio mchezo, ameweza kutambulika Baada ya kupima urefu wa mapito yake, pia kuna chatu na nyoka wenye mapembe,” alisema Dkt. Kilahama.
Aliongeza kuwa, licha ya nyoka kuhatarisha maisha ya watafiti lazima kufanyike uharaka wa kuupandisha hadhi msitu huo uwe hifadhi ya Taifa ili kuboresha usimamizi wake, “Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa Kagera (RCC), kilipitisha msitu huu upandishwe hadhi, nyoka huyu ambaye ni aina ya Giant Forest Cobra, kichwa chake kina rangi nyekundu na sehemu ya kiwiliwili rangi ya kijani. Alianza kufanyiwa utafiti mwaka 2000 baada ya kupatikana kwa taarifa kutoka kwa wenyeji wa maeneo hayo juu ya kuwepo kwa aina ya nyoka huyo katika msitu huu,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Halmashauri ya Missenyi, kupitia Maofisa wa Misitu, mwaka 2010 walianza kuweka mitego ya sindano katika mapito anayotumia ili kuchukua damu yake na kwenda kuipima vina saba ndipo ilibainika kuwa hadi kufikia mwaka huo, alikuwa na miaka zaidi ya 207.
Dkt. Kilahama alisema nyoka huyo atakuwa kivutio muhimu mkoani hapa kama atapatikana licha ya kukabiliwa na tatizo la ukumbwa wa msitu ambao hekta 25,000 kwani nyoka huyo amekuwa akihama mara kwa mara kwa ajili ya mawindo.
Ofisa Misitu wilayani hapa, Bw. Wilbard Bayona, alisema nyoka huyo ana uwezo wa kuishi siku 68 bila kula chochote zaidi ya maji baada ya kumeza mnyama yeyote ambaye atamkamata mawindoni.
---
Theonestina Juma,
Bukoba, Majira

Mkazi
wa jiji alikutwa na kamera yetu akining'inia kwenye daladala lifanyalo
safari kati ya Mwenge na Gongolamboto, bila kujali usalama wake, kama
alivyokutwa eneo la Ilala Boma, Barabara ya Kawawa Dar es Salaam jana.
(Picha na Charles Lucas) Mkazi wa jiji alikutwa na kamera yetu
akining'inia kwenye daladala lifanyalo safari kati ya Mwenge na
Gongolamboto, bila kujali usalama wake, kama alivyokutwa eneo la Ilala
Boma, Barabara ya Kawawa Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment