ASKOFU DR BOAZ SOLLO AWAONYA WACHUNGAJI KUHUSIANA NA IMANI YA FREEMASON AWATAKA WAHUBIRI NENO LA MUNGU KULIKO KUPOTEZA MUDA KUJADILI IMANI HIYO.
Askofu na kiongozi wa huduma ya Overcomers Power Centre na End Havesting Church Dr Boaz Sollo aliwaonya wachungaji wote nchini Tanzania kuachana na tabia ya kupoteza muda kufundisha juu ya kundi linaloitwa Freemason huku wengine wakidai kuwa ni Imani Fulani ambayo inataka kuteka Dunia kwa kila Nyanja kitendo kinachowafanya watumishi wengi kupoteza muda mwingi kufundisha na kufikili kuhusiana na kundi hilo na hivyo amewataka kuzidi kufundisha neno la Mungu kama inavyo takiwa.
Askofu Boaz aliyasema hayo katika ibada ya shukrani iliyofanyika katika ukumbi wa IDYDC Manispaa ya Iringa mjini siku ya jumapili ambapo katika kufundisha juu ya shukrani na namna ya kuvuta Baraka za Mungu kwa njia ya utoaji na shukrani ambapo ilikuwa ni siku muhimu sana kwa waumini wa kanisa hilo kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowetendea ikiwemo katika mavuno ya mazao,fedha pamoja na sadaka mbalimbali za kumshukuru mungu kwa yote aliyoyatenda katika maisha yao na ndipo Askofu Boaz alipotumia muda wa kuwaonya wachungaji wanaendelea na tabia ya kuendelea kufundisha imani hiyo ni sawa na kuendelea kulitukuza kundi hilo pasipo wao kujijua kwani kunyamaza kwao kunaweza kukasaidia waumini wao hasa watoto wanaokua na kulelewa na makanisa yao wasingeweza kutambua kuhusiana na kile kinacho zungumzwa juu ya kundi hilo badala yake wanakuwa huku wakisikia uwepo wa kundi hilo.
Pia katika kufundisha suala la shukrani askofu Boaz Sollo alitumia kitabu kile cha Luka 17-11-: juu ya wale kumi wenye ukoma waliohitaji kupokea uponyaji kutoka kwa yesu baada ya kukutana na Yesu nakuambiwa wakajitakase wakapona na baada ya kupona hawakukumbuka kurudi kumshukuru mungu kwa kuwa ponya na mmoja kati ya wote kumi alirudi kushukuru juu ya uponyaji alioupata na ndipo Yesu alipouliza Je,hawakupona wote kumi lakini pia zab 107 -:1 ambayo inasema mshukurunini bwana kwa kuwa ni mwema na fadhiri zake ni za milele ikiwa nisehemu ya mafundisho hayo aliyokuwa akifundisha jumapili iliyopita huku mammia ya waumini wa kanisa hilo wakimushukuru.
Askofu Dr Boaz Sollo akisoma neno la Mungu |
Askofu Dr Boaz Sollo akimfariji mtoa ushuda jinsi mume wake alivyonusurika katika ajali ya gari la Magereza Pawaga |
Mtoa ushuhuda akielezea nguvu ya maombi baada ya kuombewa na askofu Boaz Sollo kutokana na ndoto mbaya za kumpoteza mtoto huyu aliye mmbeba |
Baada ya kupona Maralia kutokana na maombezi ya Askofu Boaz Sollo |
Ushuhuda wa mtoto kupona na kuanza kutembea baada ya maombezi ya Askofu Boaz Sollo |
Huyu mama anashudia alivyo pona mkono uliomsumbua kwa muda mrefu baada ya kuombewa na Askofu Boaz Sollo |
Mama huyu akishudia juu ya amani kaika familia yake |
Askofu Dr Boaz Sollo akifundisha neno |
Askofu Boaz Sollo akitambulisha Albam mpya ya mwimbaji wa nyimbo za injili Iringamaarufu kama Mama mlowe |
Mwimbaji Mama Mlowe |
Bendi ya Jesus My Life pamoja na Askofu Dr Boaz Sollo wakiwa katika ukumbi wa IDYDC |
Mkurugenzi wa Bendi ya Jesus my Life ya Iringa |
Waimbaji wa Bendi ya Jesus my Life |
Hawa hapa mbele ni wahudumu wa Overcomers Power Centre |
No comments:
Post a Comment