Saturday, September 22, 2012

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA KITAIFA YAFUNGWA MKOANI IRINGA


 Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Iringa Ritha Motto Kabati(kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
 Mkuuwa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na Meneja Mauzo wa Airtel, Kanda ya Nyanda usini, Beda Kinunda  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa. Airtel ndio wadhamini wa maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akisalimiana na RPC wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Samora mkoani Iringa kufunga maadhimisho hayo kitaifa.
Mkuuwa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akipokea zawadi ya Airtelkutoka  kwa Meneja Mauzo wa Airtel, Kanda ya Nyanda usini, Beda
Kinunda mara baada ya kutembelea banda la Airtel ambao ndio wadhamini wakuu wa wa wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa. Kulia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani, Pereira Silima.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Mjini Bi Telesia Mahongo akiwa na Wabunge wa Viti Maalum mkoa Iringa, Ritha Motto Kabati (kulia) na  Ckiku Alfan Abwao (kushoto) wakiwa katika viwanja vya Samora mjini Iringa hii leo katika ufungaji wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa.
 Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Malangali Mkoani Iringa, Steven Mligo(kushoto) akitoa maelezo juu ya namna ya matumizi sahihi ya kufuata sheria za barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara kwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa anatembelea banda la Posili usalama barabarani jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Ofisa wa Wizara ya Ujenzi, (kulia akitoa maelezo ya Wizra hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Kushoto kabisa ni Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge
 Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Barabara TANROAD wakiwa katika banda lao
 Mkurugenzi wa Mipango wa TANROADS, Mhandisi, Jason Rwiza  (kushoto) akitoamaelezo ya taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Kulia ni kabisa ni Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge
Mneja wa Mkoa wa Iringa wa Shirika la Bima la Taifa, (NIC) Ally Mohamed (kulia) akitoa maelezo ya taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati (kushoto) na Kamanda wa Trafiki, Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga. Afisa Mauzo Msaidizi wa ASAS, Stanley Nyamle (kushoto) akitoa maelezo juu ya namna ya matumizi sahihi ya kufuata sheria za barabara kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara kwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipokuwa anatembelea banda la Posili usalama barabarani
jana katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
 Wanafunzi wakitumbuiza kwa nyimbo katikakilele hicho cha Wiki ya Nenmda kwa Usalama Kitaifa mjini Iringa hii leo.
Wabunge wa Viti Maalum mkoa Iringa, Ritha Motto Kabati (kulia) na  Ckiku Alfan Abwao (kushoto) wakifurahia jambo katika viwanja vya Samora mjini Iringa hii leo katika ufungaji wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa.  Wasanii wa kundi la Mizengwe wakitoa burudani katika sherehe za ufungaji wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaofa Mkoa wa Iringa. Kulia ni Mkaguzi wa Polisi, Abel Swai.

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Makampuni ya ASAS, Salim Abgri kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nebda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa. Abri pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Redio One na Capita Radio, Deogratius Rweiyunga kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nebda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akimkabidhi cheti Mmwenyekiti wa Kamati ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Geita, Willson Msuka kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nebda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa
Baadhi ya madereva wa Pikipiki mkoani Iringa waliopatiwa mafunzo maalum ya uendeshaji pikipiki na kufaulu wakila kiapo cha utii wa sheria za barabarani mbele ya Mgeni rasmi.
Mneja wa Mkoa wa Iringa wa Shirika la Bima la Taifa, (NIC) Ally Mohamed (kulia) akitoa maelezo ya taasisi hiyo kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma alipotembelea banda hilo. Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Ritha Kabati (kushoto) na Kamanda wa Trafiki, Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga.

IKULU:Rais jakaya kikwete alipoongoza kikao maalum cha baraza la mawaziri

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (kushoto), Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa, Waziri wa Kilimo Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki Mhe Samuel Sitta baada ya kumalizika kwa mkutano maalumu wa Baraza la Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri na Makatibu wakuu alipokutana nao Alhamisi Septemba 8, 2012 katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es salaam.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (kulia kwake) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kwake wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri na Makatibu wakuu alipokutana nao Alhamisi Septemba 8, 2012 katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es salaam.
Wajumbe katika mkutano maalumu wa Baraza la Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri na Makatibu wakuu wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) alipokutana nao Alhamisi Septemba 8, 2012 katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es salaam.

Mbeya: Baba (39) ampa mimba mwanaye (15) wa kumzaa (?!)

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya --  Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad (39), anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa (15) jina lake limehifadhiwa.

Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon (35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne, na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi  wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, Bwana Angelo Sanga.

Viongozi hao wa mtaa walimuita  mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo, lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.

Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa, waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi, ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.

Hata hivyo, hivi sasa binti huyo amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya akisubiri kujifungua ingawa umri mdogo wa binti huyo amekuwa chini ya uangalizi wa karibu wa daktari hospitalini hapo.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani Septemba 25 mwaka huu katika Mahakama kuu jijini hapa, ili kujibu tuhuma zinazomkabili katika kesi inayotarajiwa kusikilizwa na hakimu wa mahakama hiyo mheshimiwa Majige.


 

No comments:

Post a Comment