MBUNGE WA VITI MAALUM MKOAN IRINGA AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WAZAZI WA WANAFUNZI WATAKAOSHINDWA KUENDELEA NA MASOMO YA KIDATO CHA NNE MWAKANI
Wazazi na walezi mkoani Iringa wameshauriwa
kuwa karibu na watoto wao wa shule pamoja na
kujenga mahusiano mazuri na walimu ili kujua maendeleo ya watoto wao pindi
wanapokuwa shuleni.
Hayo yamesemwa na mbunge wa viti maalum mkoa
wa Iringa Mh.Litha Kabati ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika mahafari hiyo, akizungumza na wananchi
pamoja na wanafunzi katika mahafari ya tatu ya kuhitimu kidato cha nne katika
shule ya Sekondari ya Ipogolo iliyopo kata ya kitwiru manispaa ya Iringa na
kuwataka wazazi kuacha tabia ya kuwaachia walimu pekee kuwa ndiyo waangalizi wa
watoto hao badala yake washirikiane ili kuhakikisha wana tengeneza mazira
yatakayo wafanya wanafunzi wasome kwa bidii.
Aidha Mh.Litha amewataka wanafunzi kujituma
katika masomo yao pasipo kuangalia hali ya maisha katika familia zao
wanamotokea kitendo ambacho kinaweza kuharibu malengo yao kimasomo,kauli hiyo
imekuja baada ya kusomewa idadi ya wanafunzi wanaofaulu na kshindwa katika
shule hiyo ambapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 na kufikia mwaka 2008 shule
hiyo ilikuwa na kidato cha pili ambapo katika mtihani wao kati ya wanafunzi 160
wanafunzi 15 walipata C,75 D,57 F,na 13 ni watoro,2009 walikuwa 13walipata C,21
D,18 F,mwaka 2010 jumla ya wanafunzi 130 walifanya mtihani ambapo 1 alipata
C,84 D,35 F, na 10 ni watoro na mwaka 2011 wanafunzi 112 walifanya mtihani 13
walipata C,23 D,61 F,na watoro walikuwa 12 na kwa upande wa kidato cha nne kwa
mwaka 2010 -1 alipata Div III,4 Div IV,78 Div O na kwa mwaka 2011 wanfunzi 4
Div III,25 Div IV, 27 Div O, hali ambayo inaonesha mabadiliko ya kitaalima kwa
muda wa mihula miwili iliyopita.
Pia ameahidi kushirikiana na wazazi wa
wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne pale wanaposhindwa kuwapeleka watoto wao
shule hususani watoto wa kike ili kuongeza jitihada za kumkomboa mwanamke
katika hali ya kukandamizwa katika maisha lakini pia kutatua baadhi ya
changamoto zinazo ikabili shule kwa kushirikiana na wahisani wanao panda maendelea.
Akielezea changamoto zinazoikabili shule
makamu Mkuu wa shule hiyo ya Sekondari Ipogolo Bi.Hilda Gadisau amesema shule
hiyo inakabiliwa na upungufu wa maabara ya kujifunzi kwa masomo ya sayansi,ubovu
wa madarasa,upungufu wa walimu pamoja na ukosefu wa Uzio wa shule hali
inayowafanya wanafunzi kutoroka kwa
urahisi na kujiingiza katika makundi yasiyofa kama unywaji wa pombe pamoja na
uchezaji wa kamali pamoja na upungufu wa vitabu vya masomo mbalimbali ukosefu
wa jengo utawala ikijumuisha na nyumba za walimu.
Hivyo wameiomba serikali kuwasaidia kutatua
baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ilikuboresha maendeleo ya taaluma
Shuleni hapo.
Picha zote hapo chini
zinahusiana na tukio la mahafari ya kidato cha nne shule ya sekondari Ipogoro
Mgeni rasmi ni Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa hapo chiniMh.Mb.Viti maalum mkoa wa IringaLitha Kabati |
Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Ipogoro |
HS
No comments:
Post a Comment