Taarifa ya TFDA ya ufafanuzi wa taarifa mbalimbali kuhusu ARVs bandia
1.0 UTANGULIZI
a). Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii. TFDA imeweka mifumo mbalimbali ya udhibiti chini ya sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219. Mifumo hiyo ni pamoja na usajili wa bidhaa, usajili wa majengo/maeneo ya kuzalisha na kuuza bidhaa, uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za bidhaa pamoja na ukaguzi na ufuatiliaji wake kwenye soko.
b). Kupitia mifumo iliyowekwa, TFDA imekuwa ikihakikisha usalama, ubora na ufanisi wa dawa katika soko. Aidha, mifumo hiyo pia huwezesha kubaini uwepo wa bidhaa bandia na duni kwenye soko na kuchukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria. Hatua hizo ni pamoja na kusitisha matumizi ya bidhaa husika na kuziondoa kwenye soko, kuziteketeza na kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya dola na sheria.
c). Itakumbukwa kwamba, mnamo tarehe 21 Septemba 2012, tarehe 4 Oktoba, 2012 na tarehe 10 Oktoba 2012, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilitoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa dawa bandia ya kupunguza makali ya UKIMWI yenye jina la kibiashara ‘TT-VIR 30’ toleo Na. 0C.01.85 ikiwa ni pamoja na hatua zilizochukuliwa. Baada ya taarifa hizi za Wizara kutolewa, kumekuwa na taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari zinazoleta mkanganyiko kwa wananchi kuhusu suala hili.
d). Baadhi ya mikanganyiko hiyo ni pamoja na jinsi dawa hiyo bandia ilivyobainika, kama barua za TFDA ziliwafikia Tanzania Pharmaceuticals Industries (TPI) Ltd na kama uzalishaji wa dawa bado unaendelea au la.
e). Ili kuondoa mkanganyiko ambao umeanza kujitokeza, Mamlaka inapenda kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu dawa hizo bandia ambazo matumizi yake yamesitishwa. Vilevile, TFDA inapenda kutumia fursa hii kutoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa udhibiti wa dawa nchini.
2.0 UFAFANUZI KUHUSU DAWA BANDIA YA TT-VIR 30

- TFDA ndiyo iliyobaini uwepo wa dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85 kwenye soko mnamo tarehe 28 Julai, 2012 kupitia mfumo wake wa ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa katika soko.
- Kama ilivyoelezwa katika taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, TFDA inasisitiza kwamba kampuni ya TPI Ltd iliiuzia MSD dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo.
- Nyaraka hizo pamoja na vielelezo mbalimbali zimewasilishwa kwenye vyombo vya usalama kwa hatua zaidi za kisheria.
- TFDA imesitisha uzalishaji wa dawa za ARVs za kiwanda cha TPI Ltd kupitia barua Kumb. Na. CA/C.80/222/01A/47 ya tarehe 4 Oktoba, 2012 na vile vile uzalishaji na usambazaji wa dawa zote kupitia barua Kumb. Na. CA/C.80/222/01A/55 ya tarehe 10 Oktoba, 2012.
- Barua hizo zilipelekwa kwa ‘dispatch’ katika ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya TPI Ltd iliyoko eneo la Mikocheni, Dar es Salaam na kupokelewa tarehe 04 na 10 Oktoba, 2012.
- Taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zilionesha wazi kwamba TFDA ndiyo iliyositisha uzalishaji wa dawa katika kiwanda cha TPI Ltd.
- Ukaguzi uliofanywa na TFDA kwenye kiwanda cha TPI Ltd, Arusha tarehe 12 na 23 Oktoba 2012, umethibitisha kwamba hakuna uzalishaji wa dawa unaoendelea kwenye kiwanda husika kama ilivyoelekezwa na TFDA.
3.0 MFUMO WA UDHIBITI WA DAWA NCHINI
Aidha, Mamlaka inapenda kutumia fursa hii kufafanua zaidi kuhusu mfumo wa udhibiti wa dawa nchini kama ifuatavyo;
a). Udhibiti wa dawa unazingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219, kanuni zilizowekwa, miongozo, misingi ya kisayansi (science based) pamoja na miundombinu kama vile maabara na mtandao wa ukaguzi. Mifumo ya udhibiti hujumuisha yafuatayo;-
i. Kufanya tathmini ya taarifa za kisayansi kuhusu ubora, usalama na ufanisi wa dawa, kufanya ukaguzi wa viwanda na hatimaye kusajili dawa husika.
ii. Kusajili maeneo yanayojishughulisha na uzalishaji na biashara ya dawa ikiwepo masharti ya kuwa na wataalam wa kusimamia uzalishaji.
iii. Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayotengeneza dawa, vituo vya forodha pamona na maeneo ya kusambaza na kuuza dawa.
iv. Kufanya ufuatiliaji wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa zilizosajiliwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba zinakidhi vigezo na matakwa ya usajili.
v. Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakiki usalama na ubora wa dawa zinazoombewa usajili na zile zilizoruhusiwa kutumika nchini.
b). Katika kutekeleza mifumo ya udhibiti na kwa kuzingatia misingi ya udhibiti wa bidhaa duniani, mwenye jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa ni la aliyeisajili bidhaa (marketing authorization holder) ili kuhakikisha kuwa mtumiaji hapati madhara.
c). Mifumo hii ndiyo inayoiwezesha TFDA kuhakikisha usalama, ubora na ufanisi wa dawa na pia kubaini dawa bandia na duni katika soko na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.
4.0 HITIMISHO
a). Uchunguzi zaidi wa dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85 unaendelea kupitia vyombo vya usalama kwa hatua zaidi za kisheria.
b). TFDA itaendelea kufuatilia usalama, ubora na ufanisi wa dawa kwenye soko kupitia mifumo iliyowekwa ili kulinda na kudumisha afya ya jamii;
c). Tunapenda kuwakumbusha wote wanaojihusisha na biashara ya dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyowekwa na kwamba yeyote atakayekiuka taratibu hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
d). Tunawahakikishia wananchi kwamba dawa za ARVs zilizoko katika vituo vya kutolea huduma za afya ni salama na hivyo waendelee kuzitumia bila wasiwasi wowote.
e). Tunatoa rai kwa vyombo vya habari, watoa huduma za afya na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapobaini au kuhisi kuwepo kwa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba vyenye mashaka au uvunjifu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219.
Hiiti B. Sillo
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
30 OKTOBA, 2012
-----
agustnews.blogspot.com imenukuu taarifa hii kutoka wavuti.com

MbeyaYetu blog: WANAFUNZI WA DARASA LA TATU AJINYONGA KWA KUTUMIA KAMBA YA VIATU
Picha, Habari kutoka kwa Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iwambi, darasa la tatu Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.
Tukio hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa 5 kamili usiku wakati wazazi wote wa mtoto huyo Bwna Patrick Mwakapalila (52) na Bi Subira Patrick (30) wakiwa hawapo nyumbani na kwamba baba mzazi akiwa na mwanae wa kiume aitwaye Joshua Patrick (10) waliondoka majira ya saa 3:30 kuelekea mjini.
Aidha Baba wa mtoto huyo alipigiwa simu na mtu mmoja kwamba arejee nyumbani na yeye pasipo kuchelewa alirejea na kumkuta mwanae amejinyonga katika bomba la maji kwa kutumia kamba ya viatu na chini kukiwa na ndoo, ambapo kifo hicho kimezua maswali mengi kwani kimo cha mtoto ni zaidi ya futi mbili na nusu na urefu wa kamba hali inayotia shaka kuwa mtoto huyo alichukua uamuzi huo yeye mwenyewe.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ivwanga Bwana Chonde Kalisto amethibitisha tukio hilo la kusikitisha na kwamba yeye alipokea taarifa kutoka kwa Balozi wake Bi Esther Mahenge ambapo walitoa taarifa polisi ambapo walifika eneo la tukio kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

SongeaHabri blog: APIGWA MSHALE NA KUFA PAPO HAPO -SERENGETI
MWANAFUNZI WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHALE
Imeandikwa na Anthony Mayunga-Serengeti.
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe kata ya Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas Wambura(17)anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani Chacha Damiani Mangali(18) na kufa papo hapo.
Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26, majira ya saa 2 mwaka huu usiku nyumbani kwa marehemu Mangali limethibitishwa na uongozi wa kitongoji na polisi linahusishwa na wivu wa kimapenzi.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango atoke nje ya nyumba yake.
“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana huenda wamegongana kwa wanawake, maana inaonekana marehemu alifungua mlango akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga kelele kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.
Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka kama kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea kusiko julikana.
“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa na kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu aliamua kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya kawaida”alisema.
Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo ameyasikia.
“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya wanawake mara nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na majilani, nilipigiwa simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio hilo, tunaendelea kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila hata kuwaeleza sababu”alisema.
Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.
Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili Mugumu sekondari wilayani wilayani hapa Mwang’omba Kegocha(16)amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta (29)
Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali ambapo mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu ths 5,000 na katikakudaiana wakakorishana ndipo akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.

Baadhi
ya mashuhuda wakiwa wamekusanyika kushuhudia Mwili wa Mkazi wa
Kitongoji cha Gezaulole, Kijiji cha Haporoto Kata ya Ihango Wilaya ya
Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya Mbwiga Mwandele(50 -55) amejinyonga kwa
kutumia mkanda wa Suruali yake katika Ofisi ya kijiji hicho. (Picha:
Ezekiel Kamanga, Mbeya)
Gazeti la HabariLeo: VISU VYAKATIZA UHAI KWA WIVU WA MAPENZI
WAKATI mvuvi kutoka Kambi ya wavuvi ya Kakoma – Kilangawana katika Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Evod Luvanga (32), akidaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu akimtuhumu kumdhalilisha, mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam, amemchoma kisu na kumuua mchumba wake kwa sababu za kimapenzi.
Luvanga anadaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu ubavuni akimtuhumu kumdhalilisha mbele ya rafiki zake kwa kumdhihaki kuwa mkewe ni ‘mzinifu aliyekubuhu’.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha mauaji hayo yalitokea juzi katika kambi hiyo ya wavuvi usiku wa manane, ambako mtuhumiwa anadaiwa kumuua kwa kumchoma kisu ubavuni mkewe aitwaye Ales Mwanja (20) na kumsababishia umauti.
Kwa mujibu wa baadhi ya wavuvi kutoka kambi hiyo, walidai mtuhumiwa wivu dhidi ya mkewe ulikuwa ukiwaka kwa nguvu ndani yake, kwani alidai anampenda sana na hatakuwa tayari katika maisha yake kusikia ana mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine zaidi yake.
Inadaiwa kuwa kutokana na tabia yake hiyo ya kujigamba kumpenda sana mkewe, wenzake walianza kudhihaki iweje ampende kiasi hicho mkewe wakati ni ‘mzinifu’, hali iliyomkwaza mtuhumiwa ambaye aliahidi kuifanyia uchunguzi wa kina dhihaka hiyo.
“Kuanzia hapo tulimsikia mwenzetu huyu daima akilalamika kuwa mkwe si mwaminifu eti alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine hivyo aliapa ‘kumshughulikia’ ipasavyo ili wote wamkose,” alidai mmoja wa wavuvi hao.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, chanzo cha mauaji hayo ya kikatili ni wivu wa kimapenzi na kwamba Ales alifariki dunia muda mfupi baadaye kutokana na kuvuja damu nyingi. Kamanda Mwaruanda alisema mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani.
Jijini Dar es Salaam, Fatuma Selemani (21) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, amemchoma kisu mchumba wake, Selemani Ramadhani (24) mkazi wa Magomeni Somanga, na kufariki dunia akipelekwa hospitali.
Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo juzi saa saba mchana kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyela, Fatuma alimchoma kisu Ramadhani na kukimbilia kwa kaka yake aitwaye, Omary Matimbwa na kumwambia amemchoma kisu kifuani mchumba wake na anatoka damu kama maji.
Katika tukio jingine, Erasto Chalamila anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 30 hadi 40, mlinzi wa Kampuni ya Ultimate Security, mkazi wa Kinondoni Hananasif, amekutwa amekufa ndani ya chumba chake na mwili wake hauna jeraha lolote huku ukiwa umevimba ukitokwa na damu pia ukiwa na harufu kali.
Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga na Abdallah Selemani wa Polisi (OUT).

No comments:
Post a Comment