Thursday, November 1, 2012

AKUTWA AMEFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI

Mtu mmoja amekutwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha usikiwa leo katika kata ya Mwangata mtaa Muungano B Manispaa ya Iringa mjini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Bw.Maiko Kamuhanda amesema mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Abeli Nyunza mwenye umri 35 mkazi wa Kihodombi Isakalilo na dereva wa Pikipiki yenye namba T 398 CCJ aina ya Sky ford baada ya kupigiwa simu na mtu asiyemfaham majira ya usiku amfuate alikokuwa na baadaye alikutwa amefariki dunia majira saa 12 za asubuhi na kutelekezwa katika mtaro wa maji machafu,na uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini wanaohusika na tukio hilo,kamanda Kamuhanda aliwataka waendesha pikipiki kujihadhali na kuwapeleka watu wasiojulikana katika maeneo ya hatari.
Kwa upande wake Mwekiti wa mtaa huo amesema katika mtaa wake hkujawahi kutoke tukio kama hilo hivyo amewaomba waendesha pikipiki kuwa na ushirikiano katika kazi zao.

Gari ya Polisi ikiondoka na mwili waq marehem
Sehemu ambayo alilazwa marehem
Mashuhuda wakisaidia kuupakia mwili wa marehem katika gari ya Polisi
Askari Polisi akisaidiana na msamaria mwema kuutoa mwili wa marehem katika shimo
Mwili wa marehemu Abeli Nyunza ukiwa umetelekezwa katika mtaro
Mkuu wa kikosi cha upelelezi Polisi Iringa akiwa eneo la tukio mbele yake ni mwili wa marehemu

Umati wa mashuhuda wa tukio

No comments:

Post a Comment