ZAIDI YA SHULE SITA MANISPAA YA IRINGA ZANUFAIKA NA MSAADA WA KOMPYUTA KUTOKA KWA MBUNGE WA VITI MAALUM CCM MKOANI IRINGA
Katika kutimiza malengo ya mileniam pamoja na mabadiliko ya mfumo kutoka analogia kwenda Digital mbunge wa vitimaalum mkoani Iringa Bi.Litha Kabati ametoa msaada wa kompyuta katika shule saba za sekondari sita na shule ya msingi moja ambapo moja kati ya hizo ni shule iliyopo nje ya manispaa ya Iringa mjini.
Akizungumza katika utoaji wa msaada huo mbunge huyo amesema ametambua changamoto zinazozikabili shule hizo hususani ukosefu wa vitendea kazi vikiwemmo komputa pamoja na vifaa vya maabala ambapo amesema ameguswa na changamoto hizo hivyo kwa sehemu ameamua kujittolea katika kuzisaidia shule hizo akiwa ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali wanaopenda maendeleo ya elimu katika mkoa wa Iringa kutatua kero mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu mkoani humo.
Mbunge Kabati amezitaja shule zilizonufaika na msaada huo kuwa ni pamoja na shule ya sekondari Mlandege,Kwakilosa,Mtwivira sekondari,Kihesa sekondari pamoja na Shule ya sekondari Vosa Image iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini wakati kwa upande wa Shule ya msingi ni Nyumbatatu.
Ambapo amewataka walimu wa shule hizo kutumia kompyuta hizo kwa manufaa ya shule na siyo kwa maslahi binafsi.
Wakipokea msaada huo walimu wakuu wa Shule hizo wamemshukuru Mbunge Kabati kwa kutambua kero zinazo wakabili katika shule zao na kuwa msaada huo umekuja katika wakati muafaka kutokana na uhitaji wa vifaa hivyo katika urahisishaji wa kazi za shule zao pamoja na hayo wameahidi kuendeleza ushirikiano wao na mbunge kwa hali na mali na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili kusaidia sekta ya elimu ili izidi kusonga mbele.
 |
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Iringa Mh.Litha Kabati akiwa na Meya wa mmanispaa ya Iringa Mjini kushoto Amani Mwamwindi kulia ni Diwani wa kata ya Mtwivira Bw.Mushi katika ukumbi wa manispaa ya Iringa. |
 |
Miongoni mwa Kompyuta zilizotolewa na mbunge wa vitimaalum |
 |
Mbunge wa Vitimalum Mh.Littha Kabati akiwa na walimu waliokabidhiwa kompyuta |
 |
Mwalimu wa shule ya mmsingi Nyummbatatu Bi.Maria Mbilinyi akipokea msaada wa kompyuta kutoka kwa mbunge |
 |
Mkuu wa shule ya Sekon dari Kwakilosa kulia akipokea msaada wa kompyuta kutoka kwa mbunge |
 |
Mkuu wa shule ya sekondari Mlandege Bi.Asnmati Mchome kulia |
 |
Mkuu wa Shule ya sekondari Mtwivira Bw.Anton Makwaya akikabidhiwa kompyuta |
 |
Mkuu wa sekondari ya Image Vosa Iringa Vijijini akikabidhiwa kompiuta |
 |
Mkuu wa Shule ya sekondari Kihesa Bw.Hudson Luhwago kulia akipokea kompiuta |
 |
Makamu mkuu wa shule ya Efatha BwJoldan Kitosi akikabidhiwa kompiuta |
 |
Mbunge kushoto Meya katikati na kulia ni Mh.Diwani kata ya Mtwivira |
 |
Mbunge Litha Kabati akizungumza baada ya ugawaji wa kompiuta kwa kila shule |
 |
Wakwanza kulia ni Diwani wa Kwakilosa akiwa na walimu wa shule ya sekondari Efatha |
 |
Walimu |
 |
Walimu |
 |
Mwandishi wa Nuru Asia Mohamed |
 |
Katibu wa Mbunge akiangalia Komputa zilizotolewa na Mbunge |
 |
Miongoni mwa komputa zilizotolewa msaada na kwa walimu |
No comments:
Post a Comment