KKKT DAYOSISI YA IRINDA YAFANYA HARAMBEE YA KUCHANGIA VYOMBO VYA MUZIKI VYA KWAYA YA MUHIMIDINI YA KANISA KUU LA KKKT IRINGA MJINI LEO HII KATIKA PICHA . NA NI ZAIDI YA MILIONI KUMI NA TISA ZIMEPATIKANA IKIWA NI AHADI NA FEDHA TASLIM HUKU LENGO LILIKUWA NI KUPATA MILIONI KUMI NA TISA
Harambee hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki katika Kanisa Kuu
la KKKT Iringa na mgeni Rasmi alikuwa
Dk. Peter Dalali Kafumu akisindikizwa na wabunge wa viti maalum Martha Mlata na
Lita Kabati na kufanikisha harambee hiyo kuweza timiza lengo la shilingi
milioni 19 zilizohitajika kununuia vifaa vya muziki.
Kafumu katika harambee hiyo aliweza kuchangia kinanda chenye
thamani ya shilingi laki 7 na shilingi milioni 1 papo hapo na mbunge wa viti
maalum Mkoa wa Iringa Lita Kabati alichangia vifaa vya muziki vya Snake Wire na
Solo Effect vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki 6 na shilingi laki 2 papo
kwa papo na Martha Mlata alichangia shilingi laki 9.2.
BABA ASKOFU DR. OWDENBURG MOSES MDEGELLA AKIWAKARIBISHA WAGENI
MH. RITTA SEMOTTO KABATI MBUNGE VITI MAALUM AMBAYE NI MLEZI WA KWAYA HIYO AKIWATAMBULISHA WAGENI ALIOFUATANA NAO
HAPA NI MH. MARTHA MLATA AKIJITAMBULISHA
MH. DR. PETER KAFUMU MBUNGE WA IGUNGA AMBAYE NDIYE MGENI MGENI RASMI KATIKA HARAMBEE HIYO
MHE. MARTHA MLATA AKIMSIFU MUNGU KWA WIMBO WAKE "USEMAO UHIMIDIWE MUNGU WETU HALELUYA, MATENDO YAKO NI YA AJABU"
MH. DR. KAFUMU AKIFURAHIA JAMBO NA MH. RITTA KABATI HUKU HARAMBEE IKIENDELEA
HAYA NI CHANGIZO SASA
MH. DR. PETER KAFUMU AKITOA MCHANGO WAKE YEYE,FAMILIA NA MARAFIKI ZAKE
BABA ASKOFU AKIONESHA UMAHIRI WAKE KATIKA KUIMBA
No comments:
Post a Comment