TAHEA YAJITOSA KUWASAIDIA WANANCHI MKOANI IRINGA KUJITAMBU
Ili kusaidia jamii
kuondokana na adui umasiki shirika
la kitaalamu na kisayansi katika nyanja za Kilimo,Elimu, Maendeleo ya jamii na
Ustawi wa jamii{Tanzania Home Economics Association(TAHEA)}limesema liko
tayari kumsaidia mtu binafsi, familia na
jamii ya Tanzania kwa ujumla kijamii na kiuchumi kwa kutoa elimu ya fani
mbalimbali.
Hayo yamesemwa na mratibu wa shilrika hilo bw Peter
Mapunda,wakati alipokuwa akizungumzia mipango ya TAHEA,inayotekelezwa kwa sasa
ambao ni Mpango wa kuhudumia watoto waishio katika Mazingira hatarishi.
Mradi
wa kuhudumia watoto waishio katika Mazingira hatarishi ngazi ya jamii katika
wilaya ya Iringa umefadhiliwa na watu wa Marekani kupitia shirika la Africare
pamoja na mpango wa Kujengea uwezo AZAKI unaotekeleza Mpango wa Pamoja Tuwalee wa
kusaidia watoto waishio katika Mazingira hatarishi mikoa
ya Iringa Njombe, Dodoma na Singida
Aidha bw
Mapunda amesema Katika huduma ya elimu ya chakula na lishe watoto 6418 kati yao
wakike wakiwa 3105,walifikiwa kupitia walezi wao huku watoto 405 wakiume 205,na wakike 200 walisaidiwa chakula na watoto wengine 520,waliopo
chini ya miaka mitano walihakikiwa kuangalia hali ya lishe.
Hata hivyo mratibu huyo ameongeza kuwa kwa mwaka 2013
walihamasisha uundwaji wa vikundi vya kuweka na kukopa na vile vya uzalishaji mali pampja na kutoa
elimu ya chakula na lishe.
CCM, Chadema waikaba NEC Iringa
Vyama vya
siasa vilivyo na wagombea wake katika jimbo la kalenga vimeaswa kuteuwa
mawakala wanaoelewa hatua zote muhimu za uchaguzi vituoni kuanzia hatua
ya kufungua kituo hadi kutangaza matokeo,na tume imeandaa vitabu vidogo vya
maelekezo kwa ajiri ya mawakala.
Rai
hiyo imetolewa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji mstaafu Damiani
Lubuva wakiti alipokuwa akihutubia katika mkutano wa tume na viongozi wa vyama
vya siasa uliofanyika katika ukumbi wa siasa ni kilimo manispaa ya
iringa,ambapo amesema kuwa ni vyema viongozi wa vyama vya siasa wakateu
mawakala toka katika eneo husika ili kutambua vyema uhalali wa wapiga kura.
Aidha
amesisitiza kwa vyama vya siasa kuacha kutumia lugha zenye maneno ya uchochezi
na uvunjivu wa amani,na wawaase wananchi kuondoka eneo la kupigia kura mara
baada ya kupiga kura kwani kura zitakuwa salama kwakuwa kutakua na ulinzi wa
kutosha hivyo sio kila mmoja ataweza kufika katika eneo la kupigia kura
bila utaratibu .
Katika
mkuno huo uliohudhuliwa na wadau mbalimbali akiwemo kamanda wajeshi la polisi
mkoa wa iringa,kiongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,ndicho
kilicho anza kuchangia ambapo mwakilishi wake Singo Kigaila ambae ni mkuu wa
kampeni wa chama hicho amesema kumekuwa na tofauti katika daftari la wapiga
kura kuwa imeoneka katika kituo cha kaningo’mbe wameongezeka wapiga kura
watatu,ambapo hali hiyo imejitokeza pia katika vituo vingine kati ya vituo
vyote 216,vya kupgia kura.
Akijibu
hoja hiyo naibu katibu wa tume na mkuu wa IT,Dr Sisti Karia,amesema hali hiyo
ilijitokeza kutoka na marekebisho ya kasoro ikiwamo kwa wale
waliojiandikisha zaidi ya mara moja pamoja na wale waliojiandikisha mwaka
2010,na hawakuwekwa kwenye kumbukumbu hizo ndio imepelekea mabadiliko hayo.
Kwa
upande wa mwakilishi wa chama cha mapinduzi CCM,katibu wa ccm wilaya ya mufindi
bw Miraji Mtatulu ambae pia mratibu wa kampeni za chama hicho,amesema ni vyema
uongozi wa tume ukakaa tena na viongozi wa vyama siasa ili wakaangile tatizo
hilo la kuongozeka au kupungua kwa idadi ya wapiga kura na wakatoa tamko la
pomoja .
Akizungumzia
hali ya usalama katika shughuli nzima ya kampeni,kupiga kura hadi kutangazwa
kwa matokeo kamanda wa polisi mkoani iringa Ramadhani Mungi amesema siku ya
kupiga kura hatawavumilia ama kuwa ruhusu vikundi vya ulinzi vya Grini gadi au
redi gadi kuwepo eneo la kupgia kura,na atahakikisha hakuna gari yoyote itakayo
husika kubeba wapiga kura kwa namna ya kushawishiwa na mtu au chama chochote.

No comments:
Post a Comment