BENKI YA WANANCHI MUFINDI (MuCoBa)NI KIVUTIO KWA WAJASLIAMALI NYANDA ZA JUU KUSINI
Meneja Mkuu Mpya wa Benki ya MUCOBA Bw Ben Mahenge akisoma taarifa ya benki kwa wanachama wa benki hiyo |
Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa MUCOBA BENKI Bi Marcellina Mkini baada ya kuwasilisha taarifa ya meneja wa wanahisa |
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Everlista Kalalu akizungumza na wanachama wa hiza za MuCoBa Benki |
Wanachama na wanahisa wa MuCoBa |
Benki ya wananchi Mufindi(MuKoBa) imeendelea kuimarisha huduma zake ili kiwarahisishia wananchi wa mkoa wa Iringa kutunza fedha na mikopo rafiki.
Haya yamesemwa katika taarifa ya iliyowasilishwa kwa wanachama wa Benki hiyo katika mkutano mkuu uliofanyika mjini Mafinga ikiwasilishwa kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi ya Benki hiyo Bw Attilio Mohele mjumbe wa Bodi hiyo Bi Marcellina Mkini amesema wananchi wameendelea kunufaika na huduma za MuKoba huku akielezea mafanikio yanayopatikana kutokana na uboreshaji wa huduma.
Amesema wameendelea kutoa huduma za akiba na mikopo kwa kuongeza mwitikio wa uwekaji wa akiba na utumaji wa fedha,bima na matumizi ya teknolojia inayorahisisha huduma hiyo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kwa wakati pia ameelezea mikakati ya kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji wa huduma za kifedha ili kurahisha huduma kwa jamii.
Aidha Bi Mkini ameelezea changamoto zinazokwamisha maendeleo ya huduma hiyo kuwa ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa vibali vya mbao na kushuka kwa bei za mbao kutokana na ushindani,udogo wa mtaji,mkopo chechefu na gharama kubwa ya kufikisha huduma ya fedha kwa wananchi walipo vijijini.
Hivyo amewataka wananchi kuwa wavumilivu pindi wanapokuta na changamoto pindi wanapoenda kupata huduma za kifadha katika benki hiyo kwani lengo la MuKoBa ni kuwasadia wananchi wa mkoa wa Iringa.
SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI IMEKUWA TISHIO KWA WANAWAKE NCHINI
![]() |
Mkurugenzi wa T-Marc Tanzania Diana Kisaka akizindua mradi wa kupambana na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake mkoani Iringa. |
![]() |
Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa na aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo Wamoja Ayubu akitoa maoni yake |
Wanawake
Mkoani Iringa wametakiwa , kuchukua tahadhari hatua kwa kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani ya mlango
wa kizazi, ugonjwa unaoonekana
kuwa tishio kwa wanawake Wengi hapa nchini.
Akizungumza
na Mtandao huu ofisini kwake Mwenyekiti wa mabalozi wa wahudumu wa kujitolea katika
shirika la (TALWORK) Mkoani
Iringa Bw Nasri Mwampeta
amesema kuwa takwimu zinaonyesha
kuwa wanawake 2 hufariki kila
mwezi Mkoani Iringa kutokana na ugonjwa
huo ambapo kwa mwaka hufariki 24.
Amesema kuwa
ugonjwa huo unatokana na virusi
aina ya Human Papiloma Virus (H.P.V) ambavyo
huambukizwa kwa njia ya kujamiiana.
Aidha
amesema kuwa ugonjwa huo unawapata wanawake walio na umri
wa miaka (25-50) ambapo hauna dalili
kwani hukaa miaka (10-20)
baada ya hapo ndipo dalili zinaanza kujitokeza.
Ametaja visababishi vya
ugonjwa huo kuwa ni utumiaji wa
bidhaa za tumbaku, kuzaa watoto zaidi
ya watano, kujamiiana katika umri mdogo ambapo amesema kuwa wanaoishi na virusi vya ukimwi wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani.
Amewataka wanawake
kujitokeza kwa wingi kupima kwani ugonjwa huo unatibika bila
gharama yoyote katika vituo
mbalimbali Mkoani Iringa ikiwemo
Hospitali ya Mkoa, kituo cha
afya Ipogoro, Marie Stopers na hospitali ya Ipamba.
No comments:
Post a Comment