ELIMU YETU YA TANZANIA INAKWENDA WAPI?
![]() |
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa |
Hivi ni kweli kuwa elimu ni
ngumu ama mfumo wa elimu tuliojiwekea hapa kwetu ndo unaoleta ugumu katika
swala zima la elimu TANZANIA?
Mimi sijui, lakini yale ninayo
yasikia kutoka kwa watu mbalimbali ndo yaliyonifanya mimi hadi kufikia
kujiuliza swali kama hili.vijana wengi waliopo mashuleni na vyuoni wamekuwa
wakilalamika juu ya ugumu wanaokutana nao katika masomo yaho hadi kufikia
kusema kuwa elimu ni ngumu.huku ugumu huu ukionekana kuongezeka na kiwango cha
ufaulu kupungua sambamba na mabadiliko mbalimbali katika mitaala ya kufundishia
wapo waliojaribu kusema itakuja kufika siku TANZANIA kuongozwa na mtu mwenye
ufaulu wa kiwango cha zero kabisa.huku shule za serikali zikionekana kuboronga
kwa wingi hasa hizi za kata wanafunzi wanaotoka katika shule hizo
wamedai kuwa ukosefu wa vifaa
vya kufundishia pamoja na walimu kutoingia kwenye vipindi ndiko kunakochangia
wao kufanya vibaya.
kwa uchunguzi mdogo tu walimu
wengi wamekuwa wakiacha kufundisha na wanapo ulizwa kwanini wanafanya hivyo
hudai ni kutokana na kutolipwa mishahara yao kwa wakati jambo linalowafanya wao
kuwa na maisha magumu huku wengi wao wakiwa ni wapangaji katika nyumba za watu
binafsi..kitu kinacho wafanya wengi wao kufungua masomo ya ziada ama kwa jina
lingine tution ili waweze kupata fedha za kujikimu na mahitaji yao na hapo
ndipo wale wanafunzi waliopo shule hujikuta hawasomi kwani mwalimu hayupo shule
bali kwenye kituo chake cha kufundishia masomo ya ziada na ndipo wale wenzangu
na mimi wasio na uwezo wa kulipia masomo hayo hujikuta wameachwa njiani..sasa
kwa mfano mdogo kama huu ni kweli kuwa elimu
ni ngumu ama mfumo wa elimu ndo mgumu? Hii ni changamoto tosha kwa selikari
yetu kuhakikisha inaliweka sawa hili ili kuleta tija kwa wanafunzi na kufanya
kiwango cha ufaulu kuongezeka.
Baadhi ya watu wamekuwa wakichangia kupitia kipindi cha tujadili kinachorushwa na Overcomers Fm Redio kuanzia saa moja kamili hadi saa tatu asubuhi kuhusiana na chamoto ambazo walimu katika sektam ya elimu wamekua wakikabiliwa nayo ni pale tu wanapo kosa kuthaminiwa lakini pia serikali kushindwa kuwapa kipao mbele katika mishahara na kuwafanya walim kuanza kujishughulisha na mambo yatakayo waletea mafanikio kuliko kusubiri ahadi za serikali zisizo tekelezeka kwa wakati,Nini cha kufanya ni serikali kuwa thamini walim na kutambua kama ilivyo kwa sekta zingine kama vile afya,kilimo,maji umeme na nyinginezo
No comments:
Post a Comment