Thursday, June 28, 2012



VIJANA WAMESHAURIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA BIASHARA IRINGA(RETCO)ILI KUEPUKA KUHANGAIKA NA KUTAFUTA AJIRA BAADA YA KUHITIMU MASOMO YAO.
Mkuu wa Chuo Cha biashara Iringa RETCO Bw.Mwakabungu
Makamu Mkuu wa Chuo cha biashara Iringa RETCO Bw.Nchimbi akifafanua juu ya mada iliyojadiliwa na wanachuo


Miongoni mwa wachangiaji wa mada katika Chuo cha RETCO pamoja na walimu


Mwalimu Laulens Nehemiah akielezea kuhusiana na mada iliyojadiliwa na wanafunzi wa Chuo cha RETCO


Mariam Shabani wanafunzi wa RETCO akichangia hoja katika mdahalo


Ammos Ernest mwanafunzi wa Chuo cha RETCO akitetea hoja




Cecilia Ngowi mwanafunzi wa RETCO pia akichangia hoja katika mdahalo



Jackson Moris mwanafunzi wa chuo cha RETCO Iringa akichangia hoja


Wakwanza kulia ni mwalimu wa chuo cha RETCO na watatu kushoto ni mwalimu pia


Miongoni mwa wanafunzi wa chuo cha biashara RETCO Iringa wakiwa katika mdahalo

Vijana mkoani Iringa wametakiwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya Elimu ya juu kikiwemo chuo cha RETCO of Business Iringa ili kujikwamua na kuondokana na umaskini unaozikabili jamii nyingi kutokana na kukosa elimu itakayoweza kuwaondoa katika maadui watatu ambao Ujinga,Njaa na Maradhi.

Rai hiyo imetolewa na Makamu mkuu wa chuo cha RETCO Bwana Nchimbi wakati akichangia mada katika mdaalo wa wanafunzi na Overcomers Fm redio kwa kushirikiana na Mtandao wa agustnews.blogspot.com kuhusiana na mtazamo hasi wa vijana walio wengi wanaojiunga na vyuo kwa kutegemea kuajiliwa na Makampuni,mashirika,taasisi pamoja na maeneo mengine ambayo wanafikiri kupata mitaji kwaajili ya kujiajili,mwalimu huyo amesema kuwa ni vema vijana kuanza kujitambu na kutambua umuhim wa kujiunga na chuo cha RETCO kinachotoa mafunzo kwa vijana ili kuwawezesha kutambua mbinu zitakazotumika kupata mitaji kwaajili ya kujiali amesema ni vema kijana akatambua umuhim wa kujiajili wenyewe kuliko kuajiliwa katika sekta binafsi.

Akizungumzia umuhim wa kujiajili amesema kuwa inamuwezesha kujiamini katika ufanyaji wa kazi kwa lengo la kutafuta faida na mafanikio yasiyo na mashariti wala usumbufu wowote ambapo hii amesema nikutokana na ukosefu na upungufu wa ajira nchini jambo ambalo linasababisha vijana wengi wasomi kubaki bila kazi baada ya kuhitimu elimu zao wamekuwa wakizunguka kutafuta kazi za kmufanya bila mafanikio,hivyo kuwafanya vijana wengi kukata tamaa ya kuendelea na masomo.

Pia Nchimbi ameongezea na kuhusiana na vijana wengi kufikili kurudia mitihani kwa kufikiria kwenda nda vyuo vikuu kwa kupitia kidato cha sita amesema kutokana na shughuli nzito ya kurudia mitihani ya kitato cha nne ipo njia nyepesi kupitia katika vyuo vinavyotoa diploma inayoweza kikiwemo chuo cha RETCO iringa hivyo amewashauri wazazi kutambua umuhim wa wa kuwasaidia vijana wao ili wapate elimu ya ujasilia mali itakayo wawezesha kujiali wenyewe kuliko kutegemea kuajiliwa.

Kwa upande wa wanafunzi waliohudhulia katika mdaalo huo wameshukuru uongozi wa chuo hicho kwa kuona umuhim wa kuanzisha chuo ambacho kinmawawezesha vijana kupata wasomi watakao jiajili wenyewe kuliko kutegemea kuajiliwa na watu binafsi pamoja na hayo vijana haowametumia fursa hiyo kuwashauri vijana ambao wamekatishwa tamaa na kurudia mitihani ya kidato cha nne kuwa jibu lipo katika vyuo hususani katika chuo cha Retco kwa elimu bora.

No comments:

Post a Comment