Friday, December 14, 2012

MBUNGE LITHA KABATI AWAHAMASISHA WAZAZI KUCHANGIA ELIMU ILI KUIMARISHA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU KULIKO KUSUBIRI AHADI ZA SERIKALI.

Ili kuboresha sekta ya elimu na iwe yenye manufaa kwa kizazi cha sasa na cha baadaye wazazi wamehamasishwa kuchangia maendeleo ya elimu katika shule zao za msingi na sekondari.
 Hayo yamesemwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Bi Litha Kabati alipokuwa akizungumza katika mkutano na wazazi wa kata ya Kwakilosa manispaa ya Iringa mkutano uliofanyika katika shule ya msingi Muungano ili kujadili changamoto zinazo ikabili shule hiyo na namna ya kuzitatua.

Mbunge huyo amewataka wazazi kuambua umuhim wa kuchangia elimu kwa hiari kuliko kusubiri ahadi za serikali ambazo zinaweza kuchelewesha maendeleo ya elimu ya watoto wao lakini pia amewataka kuondoa dhana ya kudhani kuwa ilimu iliyopo inatolewa bure,akilinganisha na nchi ya Kenya ambayo watu wake huchangia zaidi elimu na afya kuliko kuchangia harusi na shughuli nyingine za starehe.

Aidha amewataka kutofikiri kuwa kutoa michango ya shule ni kupoteza fedha zao au ni kuwachangia walimu kitu ambacho amedai kuwa ni kushinwa kufikiri kwa kina na kushindwa kupambanua kwa makini.

Kwa upande wa mwalimu kuu wa shule ya msingi Muungano Bwana Godlove Shawa amewataka wazazi kutambua kuwa maendeleo ya shule hiyo yanategemea zaidi michango yao ili kuzitatua chamgamoto zilizopo shuleni hapo ikiwemo ukrabati wa madarasa,nyumba za walimu,vifaa vya kufundishia uboreshaji wa Maktaba ya shule pamoja ukarabati wa vyoo vya wanafunzi shuleni hapo ili kuondoa kero zinazo wakabili wanafunzi wa shule hiyo hali inahatarisha afya za wanafunzi hao. 

 
Mbunge wa Vitimaalum Litha Kabati akizzungumza na wazazi wa Kwakilosa
Mwalimu Mkuu shule ya Muungano Bw.Godlove Shawa
Mwekiti wa mtaa wa Muungano Bw.Dembe
Afisa elimu wa kata ya Kwakilosa


Wazazi katika mkutano na mbunge wa vitimaalum
Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Iringa Bi.Litha Kabati
 
Mb.Litha Kabati akikagua vyoo vya shule ya msingi Muungano
 
Mb.Litha Kabati akipewa maelekezo darasani
Wanafunzi wa Shule ya msingi Muungano


No comments:

Post a Comment