WALIMU IRINGA NA KILOLO WASHAURIWA KUJIUNGA NA ASASI ZA FEDHA ILI KUJIKWAMUA NA WIMBI LA UMASKINI
Zaidi ya shilingi
milioni mia saba tisini na
sita,imetolewa kwa wanacha wapatao 494 wa
chama cha walimu cha akiba na
mikopo{IRINGA RURAL TEACHERS SACCOS},kama
mkopo kutoka katika chama hicho ili kuwanufaisha wanachama wake.
Hayo yamebainishwa
na mwenyekiti wa chama hicho bw Abass Kamote,wakati alipokuwa akiwasilisha
taarifa ya chama katika mkutano mkuu wa 16 wa chama hicho,ambapo pia walijadili
taarifa mbalimbali ya kamati ya usimamizi ya mwaka 2013,uliofanyika katika
ukumbi was t dominic manispaa ya iringa desemba 11 mwaka huu.
Aidha
mwenyekiti huyo ameongeza kuwa licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali katika
chama hicho,wamefanikiwa kuboresha hali zao za kijamii na kiuchumi,ikwamo
ujenzi wa nyumba bora za wanachama 152,kutoa mikopo ya sh 796,650,000 kwa
wanachama 494,pamoja na kuwa saccos bora kwa saccos za mikoa ya irinmga na
njombe.
Kwa upande
wake bw Martin Simango,akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi,waziri wa fedha mh
William Mgimwa,ambae pia ni mbunge wa jimbo la kalenga,amesema kuwa ni vyema
mwanachama awe mwaminifu katika kufanya marejesho,na kila mwalimu ajiunge na
chama hicho.
Hata hivyo
ameongeza kuwa mh waziri yupo tayari kuweza kukikopesha chama hicho,ili kila
mwanachama aweze kupata mkopo kwa wakati,na kuondoa adha ya kusubiriana katika
kuchukua mikopo.
No comments:
Post a Comment