WANANCHI IRINGA WAPONGEZWA KWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
![]() |
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerad Guninita pamoja naye katibu tawala mkoani Iringa Wamoja Ayubu wakiwa katika mkutano wa mazingira |
![]() |
Baadhi ya vitu vya maonesho katika siku ya maadimisho ya mazingira yaliyofanyika Iringa mjini viwanja vya Mwembetogwa |
![]() |
Wanafunzi nao hawakuwa nyuma kuadhimisha siku hiyo |
Wakati dunia
nzima leo ikiazimisha siku ya mazingira wananchi
Mkoani Iringa wametakiwa kuendeleaa kuyatunza,na kuyaweka katika hali ya usafi na ya
kuridhisha ambapo kwa mwaka huu Mkoa wa
Iringa umeshika nafasi ya kwanza kwa usafi
kitaifa.
Akizungumza
na wananchi kwa niaba ya mkuu wa
Mkoa katika viwanja vya Mwembetogwa Mkuu wa wilaya ya kilolo Bw Gerald kuninita
amesema kuwa yeyote
atakayeharibu mazingira ikiwemo
ulimaji holela katika vyanzo vya maji
achukuliwe hatua huku akiwataka wananchi kuacha uwindaji haramu, kutunza misitu ya asili, kuhakikisha kila kaya inapanda
miti isiyopungua 10 kila mwaka na kuwafichua wale wote wanaoanzisha moto kichaa katika
mazingira.
Aidha amesema
kuwa kila wilaya
iandae taarifa ya uzuiaji moto
kichaa hasa kipindi cha kiangazi kwani
uchomaji misitu unarudisha nyuma uhifadhi wa mazingira ambapo atakayebainika kufanya hivyo kulingana na kifungu cha
sheria ya misitu no 12 atatozwa
faini ya sh laki 3 na kanuni ya sheria
ya makosa ya jinai kifungu no 21 na 22
kitatoa adhabu ya kifungo cha miaka isiyopungua 14 kwa atakayekiuka taratibu hizo.
Naye Meya wa
Manispaa ya Iringa Bw Amani Mwamwindi
amekiri Mkoa wa Iringa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika usafi na kueleza vitu vilivyopelekea kushika nafasi
hiyo kuwa ni upandaji wa miti, maua, mpangilio mzuri wa nyumba za watu, vyuo,
shule pamoja na zahanati.
Ikiwa ni mara ya kwanza Mkoa
wa Iringa kushika nafasi hii ambayo miaka kadhaa imekua
ikishikiliwa na wilaya ya Moshi iliyopo Mkoani Kilimanjaro wakazi mbalimbali
Mkoani Iringa wameonyesha kuguswa na
suala hili pamoja na kupongeza
juhudi zilizofanywa mpaka kufikia hatua hii na kuahidi kuyatunza
mazingira na kuhakikisha yanakuwa katika hali ya usafi.
No comments:
Post a Comment