WALEMAVU WAASWA KUJISHUGHULISHA BAADALA YA KUWA TEGEMEZI
Katibu wa chama cha walemavu wa macho Wasioona katika manspaa ya iringa David mgimwa amewataka walemavu wenzake kutotegemea misaada kutoka kwa serikali bali
wajishughulishe kwa kile kidogo wanacho kipata.
Akizungumza katika kikao chao kilichofanyika katika ofisi
za walemavu wa macho mjini iringa bwana David Mgimwa ameeleza kuwa anaomba ushirikiano
na serikali kwaajili ya kuanzisha chanzo cha mapato endelevu kitakacho kuwa
kinasaidia walemavu kimaisha.
Wakati huohuo Bw mgimwa ameomba misaada kutoka kwa
mashirika mbalimbali pamoja na serikali ili kujenga kituo kikubwa cha kulelea
walemavu hao pamoja na kituo cha kutolea huduma ya elimu.
Aidha
Katibu huyo ameongeza
kwa kusema kuwa anawashauri
walemavu wote wenye uwezo kidogo kuacha kutegemea misaada kila wakati bali wajishughulishe na sekta mbalimbali za
kiuchumi kwa kile wanacho kipata kutoka serikalini na taasisi binafsi.
No comments:
Post a Comment