MRADI WA SHICS KUZINDULIWA KUTUNZA UTAMADUNI WA NYANDA ZA JUU KUSINI
Chifu wa kabila la wahehe Abdul Adam Sapi(Mfwimi) akizunguza katika mkutano wa uzinduzi wa mradi wa SHICS katika viwanja vya mwembetogwa |
Meneja wa mradi wa SHICS wa tatu kulia aliyejifunga nguo nyeupe |
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ruaha Christoph Timbuka(Katikati) |
Mradi wa Utamaduni uitwao 'Fahari Yetu' wazinduliwa Nyanda za juu kusini leo katika viwanja vya Mwembetogwa Mkoani Iringa.
Akizinduzi
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ruaha
Christoph Timbuka kwa Niaba ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Nchini Tanzania amekipongeza Chuo Kikuu cha Iringa Kupata Mradi huo na
kuwashukuru Umoja wa Ulaya kwa kuwafadhili kwa miaka hiyo Mitano.
Timbuka ameuomba mradi huo kuendelea pindi ufadhili
huo utakapoisha ili watanzania wapate kunufaika zaidi kupitia mradi huo katika kudumisha utamaduni Nchini Tanzania.(MM)
Naye Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi ameutaka mradi huo
kuenzi mila na desturi ili kutuza Historia ya Nchi ya Tanzania.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu Jan Kuever amesema kuwa, lengo la mradi
huo ni kusaidia vijana kupata ajira, kupunguza umasikini kwa kuongeza
mapato katika nyanja ya utalii kwa kuelimisha wananchi wa nyanda za juu
kusini kutembelea vyanzo mbalimbali vya utamaduni uliomo Nchini
Tanzania.
Ameongeza
kuwa, Mradi huo umeshirikisha watu mbalimbali kikiwemo Chuo Kikuu cha
Iringa, TANAPA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Manispaa ya Iringa pamoja na
wananachi kwa ujumla.
Aidha,
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Prof. Nicholas Bangu ameshukuru kupata
mradi huo kupitia Shirika la Umoja wa Ulaya na kuahidi kuendeleza mradi
huo pindi mkataba utakapoisha kwani ni ufadhili wa miaka mitano kuanzia
sasa.
No comments:
Post a Comment