MKUU WA MKOA WA IRINGA:
WANANCHI JITOKEZENI KUCHANGIA DAMU
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akizungumza na wanahabari juu ya maadhimisho ya Uchangiaji wa damu salama. |
Wananchi
Mkoani Iringa wameombwa kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya kuchangia
damu kwa hiyari ili kunusuru maisha
ya wagonjwa wanaopungukiwa na damu mkoani hapa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake amesema kuwa kampeni hiyo ya uchangiaji damu ilianza june 1 na itamalizika tar 14 June mwaka huu katika viwanja vya Mwembe Togwa ikiwa lengo kubwa ni kuwa na hazina kubwa ya damu ya kutosha katika hospitali ya Rufaa.
Amesema pamoja na maadhimisho hayo ambapo mkoa wa
Iringa umebahatika kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ya siku ya uchangiaji wa
damu duniani kikanda ikiwa imebeba kauli mbiu inayosema “DAMU SALAMA UHAI WA MAMA”(SAFE BLOOD FOR SAVING MOYHERS)
Aidha ametanabaisha kuwa vifo vingine vya akina
mama katika Hospitali nyingi hapa nchini husababishwa na ukosefu wa damu iliyo
salama hivyo kila mtu aguswe na hilo kwani hakuna kama mama.
Pia Dr Ishengoma ameyataja makundi yanayohitaji
damu kuwa na pamoja na watoto wadogo waliochini ya umri wa miaka mitano
(50%),wajawazito na wanawake wenye matatizo ya uzazi (30%),Majeruhi wa ajali
mbalimbali hasa ajali za barabarani na watu wanaofanyiwa tiba ya upasuaji(15%)
na wale wote wenye magonjwa mbalimbali yanayosababisha upungufu wa damu(5%)
Hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi
katika siku hizo za maadhimisho ili kuonesha ushirikiano na kuchangia damu
ambayo na uhai wa mama.
Kwa upande wake meneja wa Damu salama salama kanda
ya nyanda za juu kusini Dr Kokuhabwa Nukuras Amesema kuwa jopo
la wataalam wa damu tayari limewasli mkoani Iringa ili kufanikisha maadhimisho
hayo ikiwa ni pamoja na kupita katika baadhi ya maeneo kuzungumza na jamii
ikiwemo mashuleni na vyuoni huku wakihamasisha kujitokeza katika uchangiaji huo
wa damu.
Aidha Dr Kokuhabwa amesema kwa kuwa katika ukanda
wa kusini hazina ya damu iko Mkoani Mbeya hivyo imekuwa
ikileta usumbufu pindi wanapopungukiwa na damu
katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa hivyo jambo linalofanyika ni
kukusanya damu ili kuwepo na hazina ndogo ya damu mkoani hapa.
Pia Dr Kokunabwa amesema changamoto iliyopo ni
elimu duni kwa jamii juu ya uchangiaji wa damu salama.
Hivyo amewaomba wananchi kuwa wazalendo katika tukio hilo kwani
watapimwa kwanza ndipo zoezi
litaendelea ambapo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili hazina ya Mkoa wa Iringa iwe na damu ya
kutosha.
No comments:
Post a Comment