Friday, June 20, 2014

VIJANA WA VIKAE IRINGA WAPEWA SEMINA YA UJASILIAMALI

Tuesday, June 17, 2014

MTOTO WA AJABU AZALIWA MAKETE

Mtoto wa ajabu amezaliwa huko wilayani makete mkoani njombe usiku wa kuamkia tarehe kumi na saba june 2014.
Ukimuona mtoto ngozi yake ni kama amevaa koti kubwa kushinda uwezo wa mwili wake akiongea na blog hii reporter Daima kyando alisema mtoto huyo wa ajabu alikua na tumbo kubwa lililomeza viungo vingine vya mwili kama miguu,mikono,kiuno na shingo.
Habari zaidi zinasema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa amekwisha fariki na alizaliwa kwa njia ya upasuaji,chanzo cha tatizo la mtoto huyo hakikuweza kufahamika mara moja mpaka tunaenda mtandaoni madaktari walikuw wakiendelea na uchunguzi.

Mama wa mtoto huo hakuweza kuongea lolote zaidi alilia kwa uchungu kwani na yeye alishikwa na bumbuazi juu ya kilichotokea akihisi ni ndoto.
 ukimuangalia zaidi mtoto huyo unaweza kugundua kuwa ana umbo la chura,eeeeh mungu heal the world.

Tuesday, June 10, 2014

Maadhimisho ya uchangiaji wa damu salama kufanyika Viwanja vya mwembetogwa manispaa ya Iringa..



MKUU WA MKOA WA IRINGA: 
WANANCHI JITOKEZENI KUCHANGIA DAMU
 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akizungumza na wanahabari juu ya maadhimisho ya Uchangiaji wa damu salama.
Wananchi  Mkoani Iringa  wameombwa  kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya kuchangia  damu kwa hiyari  ili kunusuru  maisha  ya  wagonjwa  wanaopungukiwa na damu mkoani hapa.

Wito huo umetolewa na Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake amesema kuwa  kampeni  hiyo ya uchangiaji damu ilianza june 1 na itamalizika tar 14 June  mwaka huu katika  viwanja  vya Mwembe  Togwa  ikiwa lengo kubwa  ni kuwa na hazina  kubwa ya damu ya kutosha  katika  hospitali ya Rufaa.
Amesema pamoja na maadhimisho hayo ambapo mkoa wa Iringa umebahatika kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ya siku ya uchangiaji wa damu duniani kikanda ikiwa imebeba kauli mbiu inayosema “DAMU SALAMA UHAI WA MAMA”(SAFE BLOOD FOR SAVING MOYHERS)

Aidha ametanabaisha kuwa vifo vingine vya akina mama katika Hospitali nyingi hapa nchini husababishwa na ukosefu wa damu iliyo salama hivyo kila mtu aguswe na hilo kwani hakuna kama mama.
Pia Dr Ishengoma ameyataja makundi yanayohitaji damu kuwa na pamoja na watoto wadogo waliochini ya umri wa miaka mitano (50%),wajawazito na wanawake wenye matatizo ya uzazi (30%),Majeruhi wa ajali mbalimbali hasa ajali za barabarani na watu wanaofanyiwa tiba ya upasuaji(15%) na wale wote wenye magonjwa mbalimbali yanayosababisha upungufu wa damu(5%)

Hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika siku hizo za maadhimisho ili kuonesha ushirikiano na kuchangia damu ambayo na uhai wa mama.

Kwa upande wake meneja wa Damu salama salama kanda ya nyanda za juu kusini Dr Kokuhabwa Nukuras Amesema  kuwa  jopo la wataalam wa damu tayari limewasli mkoani Iringa ili kufanikisha maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kupita katika baadhi ya maeneo kuzungumza na jamii ikiwemo mashuleni na vyuoni huku wakihamasisha kujitokeza katika uchangiaji huo wa damu.
 
Dr Kokuhabwa Nukuras Menejawa Damu salama Kanda ya nyanda za juu kusini
Aidha Dr Kokuhabwa amesema kwa kuwa katika ukanda wa kusini  hazina ya damu iko Mkoani Mbeya  hivyo imekuwa  ikileta usumbufu  pindi  wanapopungukiwa  na damu  katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa hivyo jambo linalofanyika ni kukusanya damu ili kuwepo na hazina ndogo ya damu mkoani hapa.
Pia Dr Kokunabwa amesema changamoto iliyopo ni elimu duni kwa jamii juu ya uchangiaji wa damu salama.

Hivyo amewaomba wananchi kuwa wazalendo  katika tukio hilo  kwani  watapimwa kwanza  ndipo zoezi litaendelea  ambapo amewataka  wananchi kujitokeza kwa wingi  ili hazina ya Mkoa wa Iringa iwe na damu ya kutosha.

Friday, June 6, 2014

MRADI WA SHICS KUZINDULIWA KUTUNZA UTAMADUNI WA NYANDA ZA JUU KUSINI

MRADI WA SHICS KUZINDULIWA  KUTUNZA UTAMADUNI WA NYANDA ZA JUU KUSINI

Chifu wa kabila la wahehe Abdul Adam Sapi(Mfwimi) akizunguza katika mkutano wa uzinduzi wa mradi wa SHICS katika viwanja vya mwembetogwa





Meneja wa mradi wa SHICS wa tatu kulia aliyejifunga nguo nyeupe
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ruaha Christoph Timbuka(Katikati)
Mradi wa Utamaduni uitwao 'Fahari Yetu' wazinduliwa Nyanda za juu kusini leo katika viwanja vya Mwembetogwa Mkoani Iringa.
Akizinduzi Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ruaha Christoph Timbuka kwa Niaba ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Tanzania amekipongeza Chuo Kikuu cha Iringa Kupata Mradi huo na kuwashukuru Umoja wa Ulaya kwa kuwafadhili kwa miaka hiyo Mitano.
Timbuka ameuomba mradi huo kuendelea pindi ufadhili
huo utakapoisha ili watanzania wapate kunufaika zaidi kupitia mradi huo katika kudumisha utamaduni Nchini Tanzania.(MM)
Naye Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi ameutaka mradi huo kuenzi mila na desturi ili kutuza Historia ya Nchi ya Tanzania.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu Jan Kuever amesema kuwa, lengo la mradi huo ni kusaidia vijana kupata ajira, kupunguza umasikini kwa kuongeza mapato katika nyanja ya utalii kwa kuelimisha wananchi wa nyanda za juu kusini kutembelea vyanzo mbalimbali vya utamaduni uliomo Nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa, Mradi huo umeshirikisha watu mbalimbali kikiwemo Chuo Kikuu cha Iringa, TANAPA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Manispaa ya Iringa pamoja na wananachi kwa ujumla.
Aidha, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Prof. Nicholas Bangu ameshukuru kupata mradi huo kupitia Shirika la Umoja wa Ulaya na kuahidi kuendeleza mradi huo pindi mkataba utakapoisha kwani ni ufadhili wa miaka mitano kuanzia sasa.

Thursday, June 5, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA YAFANA IRINGA TAZAMA

WANANCHI IRINGA WAPONGEZWA KWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerad Guninita pamoja naye katibu tawala mkoani Iringa Wamoja Ayubu wakiwa katika mkutano wa mazingira
Baadhi ya vitu vya maonesho katika siku ya maadimisho ya mazingira yaliyofanyika Iringa mjini viwanja vya Mwembetogwa
Wanafunzi nao hawakuwa nyuma kuadhimisha siku hiyo
Wakati  dunia nzima  leo  ikiazimisha siku ya mazingira  wananchi  Mkoani Iringa wametakiwa kuendeleaa kuyatunza,na  kuyaweka katika hali ya usafi na ya kuridhisha  ambapo kwa mwaka huu Mkoa wa Iringa umeshika nafasi ya kwanza kwa usafi  kitaifa.
Akizungumza  na wananchi  kwa niaba ya mkuu wa Mkoa katika  viwanja vya Mwembetogwa  Mkuu wa wilaya ya kilolo Bw Gerald  kuninita  amesema kuwa yeyote  atakayeharibu  mazingira ikiwemo ulimaji holela katika  vyanzo vya maji achukuliwe hatua  huku  akiwataka wananchi  kuacha uwindaji  haramu, kutunza  misitu ya asili, kuhakikisha kila  kaya inapanda  miti isiyopungua 10 kila mwaka na kuwafichua  wale wote wanaoanzisha moto kichaa katika mazingira.
Aidha  amesema kuwa  kila  wilaya   iandae taarifa ya  uzuiaji moto kichaa hasa  kipindi cha kiangazi  kwani  uchomaji misitu unarudisha nyuma uhifadhi wa mazingira  ambapo atakayebainika kufanya  hivyo kulingana na kifungu  cha  sheria ya misitu no 12  atatozwa faini ya sh laki 3  na kanuni ya sheria ya makosa ya jinai kifungu no 21 na 22  kitatoa adhabu ya kifungo cha miaka isiyopungua 14  kwa atakayekiuka  taratibu hizo.
Naye  Meya wa Manispaa ya Iringa  Bw Amani Mwamwindi amekiri Mkoa wa Iringa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika usafi  na kueleza vitu vilivyopelekea kushika nafasi hiyo kuwa ni upandaji wa miti, maua, mpangilio mzuri wa nyumba za watu, vyuo, shule pamoja na zahanati.
Ikiwa ni mara ya kwanza  Mkoa  wa Iringa  kushika  nafasi hii ambayo miaka kadhaa imekua ikishikiliwa na wilaya ya Moshi iliyopo Mkoani Kilimanjaro wakazi mbalimbali Mkoani Iringa  wameonyesha  kuguswa na  suala hili  pamoja na kupongeza juhudi  zilizofanywa  mpaka kufikia hatua hii na kuahidi kuyatunza mazingira na kuhakikisha yanakuwa katika hali ya usafi.



Wednesday, June 4, 2014



 WALEMAVU WAASWA KUJISHUGHULISHA BAADALA YA KUWA TEGEMEZI
Katibu wa chama cha walemavu wa macho  Wasioona    katika manspaa ya iringa David mgimwa  amewataka walemavu wenzake    kutotegemea misaada kutoka kwa serikali bali wajishughulishe kwa kile kidogo wanacho kipata.

Akizungumza  katika kikao chao kilichofanyika katika ofisi za walemavu wa macho mjini iringa bwana David Mgimwa ameeleza kuwa anaomba ushirikiano na serikali kwaajili ya kuanzisha chanzo cha mapato endelevu kitakacho kuwa kinasaidia walemavu kimaisha.

Wakati huohuo Bw mgimwa ameomba misaada kutoka kwa mashirika mbalimbali pamoja na serikali ili kujenga kituo kikubwa cha kulelea walemavu hao pamoja na kituo cha kutolea huduma ya elimu.

Aidha Katibu  huyo    ameongeza   kwa kusema kuwa anawashauri walemavu wote wenye uwezo kidogo kuacha kutegemea misaada kila wakati  bali wajishughulishe na sekta mbalimbali za kiuchumi kwa kile wanacho kipata kutoka serikalini na taasisi binafsi.

UONGOZI MPYA WA TFF CHINI YA RAIS MALINZI WAMUINUA MVERA KUWA MKURUGENZI WA WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI

ALIYEKUWA KATIBU WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA IRINGA ELIUDI MVELLA WAMAHANJI AJIUZULU RASMI ,SASA NI MATAWI YA JUU....
Malinzi ninaimani na Mvella atatumia uzoefu wake wa muda mrefu katika uongozi wa mpira wa miguu kuhakikisha TFF inaimarisha uhusiano wake na wanachama wake.
TFF ina wanachama 44 ambao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Aliyekuwa katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Eliud Mvella Wamahanji ambae amejiuzulu nafasi hiyo rasmi 
Wamahanji  katikati akizungunza na wanahabari mkoa wa Iringa  sababu za kujiuzulu kwake 
Wanahabari mkoa  wa Iringa wakimsikiliza aliyekuwa katibu wa chama  cha soka mkoa wa Iringa Eliud Mvela Wamahanji kulia alipotangaza kujiuzulu nafasi yake 
Wamahanji  akiwashukuru  wanahabari Iringa kwa ushirikiano wao mkubwa 

Wamahanji  akimtambulisha katibu wake msaidizi Bw Ambwene ambae atakaimu nafasi yake hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika 

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

ALIYEKUWA katibu  wa chama cha soka mkoa wa Iringa Eliud Mvella Wamahanji ametangaza rasmi  kujiuzulu nafasi hiyo na kuahidi makubwa katika  kuinua soka hapa nchini.

Sababu kubwa ya  kuitana  hapa ni kutaka  kuwaaga baada ya  kuamua kujiuzulu nafasi ya ukatibu mkoa  wa Iringa baada ya TFF kuniteua kuwa mkurugenzi msaidizi wa sheria na uanachama wa TFF nitakayosimamia kitengo cha  wanachama 44 wa TFF .
Wamahanji  alisema  kuwa baada ya  TFF kumuona anafaa kuongoza nafasi hiyo binafsi ameamua  kujiuzulu nafasi hiyo japo haikuwa lazima  kuachia ngazi nafasi hiyo.

Alisema  kuwa ni mengi amepata  kuyafanya katika soka la Tanzania na mkoa  wa Iringa na  hivyo anatambua  kuondoka kwake ni sehemu ya mafanikio ya  jitihada zake katika  kuendeleza soka la Tanzania na  kuwa hata atakapokwenda TFF katika nafasi hiyo aliyopewa atahakikisha anaendelea  kufanya  vema zaidi.

"kubwa ambalo  nimefanikiwa katika uongozi wangu ni kuzalisha  waamuzi 15  katika mkoa  wa Iringa pamoja na kuziwezesha  timu  mbili za mkoa  wa Iringa Kurugenzi na Lipuli Fc kucheza  ligi daraja kwanza"

Hata  hivyo alisema  kuwa mbali ya mafanikio hayo  pia suala la mahusiano kati ya vyombo  vya habari na serikali ya mkoa kuna  vimeendelea  kuwa pamoja .

Aidha  alisema jitihada nyingine  alizozifanya ni kuanza makakati wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa nyasi za bandia katika Manispaa ya  Iringa uwanja  utakaojengwa eneo la Kitwiru chini ya ufadhili wa FIFA na TFF na kuwa jitihada za ujenzi zinaendelea kufanyika na Manispaa ya Iringa tayari  imetoa eneo .